Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ameandika Zitto Kabwe, kiongozi wa ACT Wazalendo:
CAG akishatoa ripoti yake AMEMALIZA. Ripoti yake ni ya mwisho. Ni FINAL. Kazi inayofuata ni ya Bunge.
Umma ujue kwamba, kabla CAG hajatoa ripoti yake Serikali hupewa nafasi ya kujibu hoja za Ukaguzi. Baada ya Ripoti kutoka majibu sio kwa Serikali tena, ni kwa Bunge.
Wakati wa mchakato wa Ukaguzi Maafisa Masuuli hudharau na kuzembea kujibu hoja kwenye ‘Exit meeting’. Baada ya CAG kutoa ripoti Rasmi na kuonyesha madudu, maafisa masuuli wanalia lia.
Nimeona Waziri Jenista Mhagama na Naibu Spika Zungu wakijaribu kuzuia Wabunge kuongelea ripoti ya CAG eti kanuni haziruhusu. SIO KWELI.
Wana mislead Bunge. Siku 21 Naibu Spika anazosema Serikali inapewa NI SIKU 21 KABLA YA CAG KUANDAA RIPOTI YA MWISHO sio baada ya ripoti kutoka. Ripoti ikishatoka ni mali ya umma, inajadiliwa na kila mtu. Wabunge wana Haki hiyo pia.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ukaguzi Serikali ilipaswa kuwasilisha Bungeni mpango wa majibu ya hoja za CAG Pamoja (concurrently) na ripoti ya CAG. Serikali haijafanya hilo Kwa hiyo hawana Haki kuwazuia Wabunge kuzungumzia ripoti ya CAG.
Ni aibu kubwa kwamba wakati Umma unamsifia Rais kwa uwazi mkubwa kuhusu ripoti ya CAG, Bungeni, Wawakilishi wa Wananchi wanazuiwa kujadili eti mpaka Novemba!
Wananchi watahisi kuwa Serikali inataka kuficha kitu.
Namna Rais Samia amelishughulikia Suala la CAG report Ndio njia sahihi: Uwazi>Uhuru wa mjadala>Hasira >Hatua>Maelekezo>hatua zaidi zatakiwa!
Bunge lisizuie mjadala. Acha Watu waongelee hoja za CAG. Huo Ndio mchakato wenyewe.