Kusema kweli nipo nikisoma maoni yenu kimsingi kabisa na hayana wasiwasi juu ya uchambuzi ninaoufuatilia ,nilichokigundua ni kuzidi kumpaka matope Zitto na shutuma nyingi zinatoka kwa wafuasi wa Chadema ,sielewi kwanini leo hii Zitto amekuwa anawasababishia kichefuchefu wadau wa Chama hiki cha Chadema.
Ukiangalia kwa kina kabisa utaona wafuasi wa Chadema wapo katika mikakati ya kumuangamiza kama matarajio ya CCM yalivyo ,wammalize na asitajike katika duru za kisiasa.Yeye kuwemo katika kamati ya Raisi hatakuwa ni mtu wa mwanzo yupo Hamad Rashid mpinzani nambari one ndani ya Tanzania na ni mtu wa kuheshimika sana na CCM na Serikali yake inalielewa hilo ,pili hakuna mzozo kati ya Hamad Rashid na CUF.
Kumchukia Zitto na kumfanya si lolote si chochote na kusema kuwa ameanza kusahaulika hapo Chadema watakuwa wanalipa fadhila za kipunda ,fahamuni tu kuna vingunge kibao wamehama CUF na hatukuona mtiririko wa mawimbi yaliyochafua uhusiano kati ya nomads hao na uongozi wa CUF ,yalipita kama maneno ya siku mbili tu ambayo yakichochewa na waandishi na vitimba kwiri wengine ,lakini bahari ilitulia na leo watu wanendelea na kuheshimiana ,CUF haikuanika wala kutafuta vyombo vya habari na kumlaani aliehama zaidi ya kumtaka huyo aliehama ajiheshimu na kuheshimiana na hadi leo husikii tena maneno maneno ,ila hapa Chadema Zitto bado ni mwanachama lakini kumekuwa na masimango makubwa sana ambayo yatamfanya awe mnyonge siku zote na vile vile kuonekana si mwenye hekima ,nasema mnachomfanyia mwanachama ambae bado ni mwenzenu ni kuzidi kumhujumu na kutaka kile mlichokuwa nacho kukidhihirisha ,ukweli ambao ni ushauri wa bure ili kuzima majaribu haya aidha viongozi wa Chadema wakemee juu ya hujuma hizi au kwa Zitto kuwaepuka Chadema kwa salama na amani kabisa.
Rai niliyoitoa ni kujaribu kumrudisha Zitto kwenye chati za ulingo wa siasa ambazo kwa imani yangu zinaweza kurudi na kuzidi pale alipofikia ikiwa tu atajiunga na Chama cha CUF ,hilo halina mbadala kuliko kuendelea kuishi ndani ya jeneza la Chadema na kuonekana kama mtu aliefiliwa na kuondokewaa na wazazi wake na hana wa kumsaidia ,waChadema wote wanaonekana wamemsaliti.
Naamini kabisa kuwa vijana wengi bado wana imani nae na ikiwa atakuja kwa mshindo wa kuhamia CUF basi nawahakikishia hakuna atakaerudi nyuma katika kumuunga mkono, zaidi ya wapiga makelele na wapiga debe wa CCM na Chadema kumwandama kwa mijineno, lakini aminia kabisa nguvu ya upinzani Tanzania itakuwa kama imezaliwa upya na msukumo wake utakuwa si wa kawaida maana CUF shughuli za kupambana na wafuasi wa Sultani CCM wanaziweza na hilo mwengi wenu mnalielewa na halina ubishi.Maana kashkash za CUF hazina kurudi nyuma kilichobakia ni uamuzi wa viongozi tu ambao wamekuwa kila kukicha wakiionya serikali iliyoko madarakani isicheze na amani ya nchi hii siku CUF wakiamua kufungulia basi hakuna cha jeshi wala polisi ni lazima CCM waje na sare ya East & central Afrika ya kupika mseto ,natumai Zitto anahitajika kujiunga na CUF na hili ni jambo ambalo CCM na marafiki zake wanaliogopa kikweli.
Na WaTanzania walio wengi wanamtazama Zitto kwa jicho la tamaa kabisa ikiwa atajiunga na CUF basi mambo yatazidi kutimia.Na kutakuwa hakuna wa kulalamika kwani mambo yatakuwa ni mbele kwa mbele.