sisi wana wa kigoma tunachagua mtu mwenye uwezo na sio kwa sababu ati zitto kasema.....................umeona jimboni kwake walivyoshikana mashati na yule jamaa wa ccm.....na kama si kuchakachua basi alley wa chadema angeshinda kigoma mjini.
Mugo"The Great";1216829 said:Mwanzilishi wa post hii si mkweli na inaonekana ana chuki na Zitto Kabwe. Ni ukweli usiofichika kuwa NCCR ina nguvu sana Kigoma hasa Kasulu na Nguruka. Dada Agripina Zai wa Kasulu vijijini si mpambanaji wa leo amekuwepo tangu changuzi za nyuma ila uchakachuaji ndiyo ilikuwa issue kubwa. Hivi wewe uliyeanzisha post hii unaijua Kigoma na politics zake? I doubt. NCCR ilikuwa na nguvu hata kabla Nsanzugwanko hajaihama na kuingia sisiemu.
acha chuki na zitto
zitto amezunguka sehemu kibao akiwapigia debe chadema
well saidLabda ucaguzi huu utawafanya Watanzania muanze muwafahamu Waha, kabila lililo kubwa mkoani Kigoma na ambalo limesahaulika kabisa tangia zama za mkoloni, na tangu Uhuru wa Tanganyika. Kigoma wakiisha toa uamuzi, hawabadiliki badiliki kama bendera inayofuata upepo. Msingi wa NCCR-Mageuzi Kigoma Kusini ulijengwa na Kiffu Hussein Kiffu. Kiffu akanunuliwa na CCM, Waha wakamwambia nenda peke yako. Aligombea udiwani mara alipohamia CCM akanyimwa kura. Kipindi hicho Ruhuza alikuwa Kigoma akiongezea nguvu alizozikuta. Kafulila alipoondoka Chadema kwenda NCCR alifuata wananchi na wala siyo kwamba amechukua wana Chadema. Kasulu Vijijini nako huyo IRON LADY Agripina Zaituni Buyogera amejenga ngome imara sana (at grassroot level) ya NCCR-Mageuzi ambayo ilinyakua Serikali nyingi za Mitaa mwaka jana. Nguvu hiyo ya Iron Lady Buyogera ndiyo imezickua kata kadhaa za Kasulu na Kibondo pamoja na Majimbo matatu. Zitto Kabwe alielekeza nguvu zake Kigoma Mjini na Manyovu, majimbo ambayo Chadema imefanya vizuri sana na kwa Kigoma Mjini, wananchi wanaamini Chadema imeshinda lakini kura zao zikaibiwa. Aliyeshinda Jimbo la Manyovu Albert Ntabaliba anajua nguvu alizopambana nazo ikiwa ni panoja na Halmashauri ya Kasulu kutawaliwa na NCCR-Mageuzi na Chadema. Zitto Kabwe hajakisaliti chama cha CHadema. Hiyo ndiyo Kigoma, mkoa ambao haufifiki hasa baada ya Serikali kuua Reli ya Kati. Ninaamini kuwa NCCR-Mageuzi itaona umuhimu wa kuwa na Mwenyekiti mpya MWANAMKE ambaye amewezesha kupata viti vya ubunge vitatu. Kiffu wa CCM arudi nyumbani kwake NCCR kuendeleza Mageuzi. WAHA wameonyesha njia, Watanzania mko wapi?
Sio Chuki katoa hoja mjibuni, unajua watanzania sasa hivi wanaona vizuri ni vigumu kuwapiga changa la macho. issue kwa nini yeye kama mjumbe wa Chadema Slaa kaanguka saana kwake?
Kumbuka hata yeye mwenyewe ilibidi apambane ili kutetea Jimbo lake unadhani CCM wanapenda kumwona anarudi Bungeni na kuwasumbua sumbua usimlaumu bila sababu za msingi..
Zitto watanzania wengi sana wametoa maoni ya kukusupport hii ni ishara kwamba wewe ni moja ya resources muhimu kwa chadema na ninaamini umejariwa kutembelea nchi za wenzetu huko ulaya na mashariki ya mbali umewaona walivyo royal kwa vyama vyao na watu wao. Watanzania wangependa kukuona ukiendelea chadema.DR.SLAA ni mentor wako mzuri ambaye sisi tunaamini anaendelea kukupika ufikie kilele cha mafANIKIO KATIKA SIASA.Sisi tulio nje ya chadema tunakuonea shauku jinsi anavyokuandaa huyo mzee SLAA hakika you have a bright future within chadema sphere.BE TOLERANCE YOU GONNA FLY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!