Labda ucaguzi huu utawafanya Watanzania muanze muwafahamu Waha, kabila lililo kubwa mkoani Kigoma na ambalo limesahaulika kabisa tangia zama za mkoloni, na tangu Uhuru wa Tanganyika. Kigoma wakiisha toa uamuzi, hawabadiliki badiliki kama bendera inayofuata upepo. Msingi wa NCCR-Mageuzi Kigoma Kusini ulijengwa na Kiffu Hussein Kiffu. Kiffu akanunuliwa na CCM, Waha wakamwambia nenda peke yako. Aligombea udiwani mara alipohamia CCM akanyimwa kura. Kipindi hicho Ruhuza alikuwa Kigoma akiongezea nguvu alizozikuta. Kafulila alipoondoka Chadema kwenda NCCR alifuata wananchi na wala siyo kwamba amechukua wana Chadema. Kasulu Vijijini nako huyo IRON LADY Agripina Zaituni Buyogera amejenga ngome imara sana (at grassroot level) ya NCCR-Mageuzi ambayo ilinyakua Serikali nyingi za Mitaa mwaka jana. Nguvu hiyo ya Iron Lady Buyogera ndiyo imezickua kata kadhaa za Kasulu na Kibondo pamoja na Majimbo matatu. Zitto Kabwe alielekeza nguvu zake Kigoma Mjini na Manyovu, majimbo ambayo Chadema imefanya vizuri sana na kwa Kigoma Mjini, wananchi wanaamini Chadema imeshinda lakini kura zao zikaibiwa. Aliyeshinda Jimbo la Manyovu Albert Ntabaliba anajua nguvu alizopambana nazo ikiwa ni panoja na Halmashauri ya Kasulu kutawaliwa na NCCR-Mageuzi na Chadema. Zitto Kabwe hajakisaliti chama cha CHadema. Hiyo ndiyo Kigoma, mkoa ambao haufifiki hasa baada ya Serikali kuua Reli ya Kati. Ninaamini kuwa NCCR-Mageuzi itaona umuhimu wa kuwa na Mwenyekiti mpya MWANAMKE ambaye amewezesha kupata viti vya ubunge vitatu. Kiffu wa CCM arudi nyumbani kwake NCCR kuendeleza Mageuzi. WAHA wameonyesha njia, Watanzania mko wapi?