mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Zitto Kabwe akiongea katika kipindi cha Power Breakfast amesema kuwa “Tulitarajia kwamba mambo ya 2019 na 2020 (Kuhusu uchaguzi) yangekuwa mambo ya aibu kwamba yasingeweza kutokea tena lakini yanatokea, kwa hiyo misingi ni msingi wa kikatiba na msingi wa kisheria, ni dhahiri kwamba hatuoni tukipata katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu kwa hiyo ni lazima ujenge mazingira ambayo utakuwa na tume ambayo itawafanya watu wakichaguliwa waingie bungeni , ukilitazama bunge la Kenya na bunge la Tanzania unaona tofauti ilivyo kubwa, hata sasa hivi kwa mfano sheria ingesema majina yaende kuthibitishwa bungeni na bunge hili?”
“Kuna vitu ambavyo lazima muwe mnaiga, unapata nini wakati gani ili kwenda kupata kikubwa? Kwamba lazima ujue kutofautisha kati ya vita kubwa na ndogo, vita kubwa ni ile ambayo unaitaka ambayo kwetu sisi ni katiba mpya lakini kuna vita ndogondogo hapa katikati lazima uzishinde ili uweze kufikia vita kubwa na kuipata hiyo vita ndogo ni kuishika, mfano; Huko nyuma mpaka sasa hivi ukigombea ubunge ukamteka mpinzani wako, muda wa kurudisha fomu ukapita unatangazwa umepita bila kupingwa, sasa hivi sheria imekataza kwamba ukiwa peke yako wananchi wataenda kuamua ndiyo au hapana, tulikatae hilo? Unamdai mtu Shilingi 100 anakupa 60, ichukue kwanza tia mfukoni endelea kudai 40 zilizobakia”