Pre GE2025 Zitto Kabwe kugombea Urais wa Tanzania 2025, Jimbo la Ubunge Kigoma mjini anawaachia Vijana wa ACT Wazalendo

Pre GE2025 Zitto Kabwe kugombea Urais wa Tanzania 2025, Jimbo la Ubunge Kigoma mjini anawaachia Vijana wa ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la Mh. Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa.

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo.

My take; Lissu sasa arudi NCCR tu.

=====

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama Chama katika miaka yao 10 kama Chama chenye usajili wa kudumu, wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara kwa kumsimamisha Kiongozi wao Mstaafu wa Chama Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jussa ameyasema hayo jana katika sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 10 ya ACT yaliyofanyika mkoani Kigoma ambapo amebainisha kuwa Zitto anayo nafasi kubwa ya kukivusha chama hicho na kuchukua uongozi wa Nchi.

“Tunajua Mnamtaka Zitto kuwa Mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hilo” — Jussa.

Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu, Zitto Kabwe amesema kuwa “Niko tayari na nimejianda kimaarifa na kusaikolojia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wowote mkinihitaji niko tayari, kuhusu ubunge hakuna shida wakina Nondo wapo na Vijana wengine wakati wowote tupo tayari kuleta mabadiliko ya ya Nchi yetu, mimi ni mstaafu napokea amri kutoka nyie Viongozi wangu”.

Zitto kabwe mbali na hayo amesema miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chama hicho inatosha kukifanya kuwa Chama kikubwa Nchini na cha Watu hivyo mpango wa miaka 10 ijayo ni mkakati wa kuhakikisha Chama kinashika dola.

Kuhusu mpango wa Chama kumtaka kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025, Zitto alisema kuwa alijipanga kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini Chama kinayo maamuzi na kama kitaamua hivyo basi hatokuwa na kipingamizi.

Millard Ayo
 
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la mh Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo

Source: Mwananchi

My take; Lisu sasa arudi NCCR tu
😡😡😡😡😡
 
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la mh Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo

Source: Mwananchi

My take; Lisu sasa arudi NCCR tu
Labda uRais wa TFF
 
Urais wa wanafik tz hilo atapita hata mm nitampigia kula ila sio kua Rais wa tz ...maana sisi tunaompendaJPm alisema tukazikwe nae chato 🥶🥶
 
Back
Top Bottom