The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amezungumza kwa msisitizo kuhusu mapambano ya chama hicho kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika kwa haki, huku akiwataka wananchi wa kijiji cha Ilalanguru, Jimbo la Kigoma Kusini, mkoani Kigoma kuchagua viongozi wanaowajibika.
Akihutubia wananchi hao Novemba 21, 2024, Zitto amebainisha hatua zilizochukuliwa na ACT Wazalendo katika kudai haki ya demokrasia.
Akielezea mikakati ya ACT Wazalendo kupitia ilani yao ya uchaguzi ambayo ni maalumu kwa serikali za mitaa, Zitto ameahidi kuwa chama hicho kitarejesha uwazi na uwajibikaji katika ngazi ya vijiji. Ameeleza kuwa viongozi watakaochaguliwa kupitia chama hicho watahakikisha wanarudisha sauti za wananchi kwa kufuata maelekezo ya ilani ya uchaguzi.
Soma pia: Zitto ashauri upinzani kuungana kwenye chaguzi kuing’oa CCM
Chanzo Jambo TV
View: https://www.instagram.com/p/DCoWE6CNCvs/comments/