Zitto Kabwe: Kuna Mvutano Mkubwa kati ya Wakulima na wafugaji Mkoani Lindi na Tunduru

Zitto Kabwe: Kuna Mvutano Mkubwa kati ya Wakulima na wafugaji Mkoani Lindi na Tunduru

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa kuna mvutano mkubwa baina ya wakulima na wafugaji mkoani Lindi na Wilaya ya Tunduru kwa kile alichobainisha kuwa ni kukosekana kwa mipango ya matumizi sahihi ya ardhi kama ilivyokusudiwa.

Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Kabwe amebainisha kuwa Wilaya ya Kilwa pekee imerekodi vifo 12 vinavyotokana na migogoro hii mwaka huu.

Ameitaka Serikali kuingilia kati ili kumaliza mvutano huu.

Zitto Kabwe aliwahi pia kuhudumu kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini kati ya mwaka 2005-2015.
 
Back
Top Bottom