Zitto Kabwe: Kwaheri John Magufuli, Buriani Tingatinga

Mkuu sikutegemea mkongwe kama wewe hapa JF uandike huu ugoro.
Samahani lakini
Nani alikudanganya ukongwe ni kinga ya ugoro?

Huna haja ya kuomba samahani kiongozi wangu. Labda uiombe samahani K Vant niliyokunywa
 
Very good Zito Kabwe.

Hiyo ndivyo ninavyoamini pia kuhusu huyu jamaa.

Tofauti yangu na wewe ni katika ile aya ya mwisho namna ulivyomalizia.

"...Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi. Mungu akusamehe dhambi zako..."

Kwanza shukrani kwa kumsamehe pale alipokukosea. Mimi pia namsamehe na kumwachilia kabisa toka moyoni mwangu na sasa niko huru...

ILA: Sisi hatuna UWEZO wa kusamehe dhambi wala kumwombea sasa kwa Mungu ili amsamehe dhambi zake.

Mtu huongozwa sala ya toba ili kusamehewa dhambi akiwa hai. Sisi wakristo tunajua na kuamini kuwa BAADA YA KIFO NI HUKUMU..

Hukumu ya ADHABU YA MILELE au RAHA YA MILELE, anajua yeye Mungu maana ndiye aonaye NIA na NDANI ya moyo wa binadamu...!
 
Sahihi kabisa, Hayati alikuwa chungu tamu, mtu anayetamani kufikia mambo makubwa na anayafikia bila kujali njia aliyopita kuyafikia (consequentialist) Ndio maana tumepiga Hatua kwenye miradi mikubwa lakini kwa gharama ya kupoteza demokrasia na utii wa Katiba

Tujifunze sasa kuunda taasisi imara badala ya kushabikia "One Man army "ili mambo mazuri yaendelee hata Kama muasisi hayupo.
 
Kumbe Magu alikuwa mwema sana kwako. Kiri basi hakukuibia kura kule jimboni, au unazungumziaje kuhusu madai ya wizi wa kura?
Wanasiasa kama wanasiasa.

Hawana utu huruma Upendo wala kumbukumbu.

Vigeugeu wanaumiza mioyo ya wengi.

Tuombe Neema ya Mungu.

Usimtegemee wala kumtumainia mwanadamu.

All I can say ' IMEKWISHA.

MUNGU NI MKUU
 
Baki na imani yako hiyo hiyo. Wenzako wanaamini vinginevyo.

Tusipangiane.
Bora kila mtu abaki na imani yake, maana wengine watahoji wale wanaosombwa na mito au kuliwa na wanyama wakali ndio wamesave adhabu ya kaburini au!
 
Zitto Kabwe ni mtata mtata sana!
Zitto hawezi kuachia attention impite. Wakati wa kifo cha Maalimu alikuja na ile “niliacha kupokea simu ili nisipokee taarifa ya msiba”. Mtu ambaye msiba si mgeni kwake maana amewahi kufiwa na hadi mama mzazi.

Leo, “nilikuwa simchukii...” wakati tunakumbuka mwaka 2019 alishabikia uzushi wa kifo cha Jpm kwenye mitandao..
 
Kaburini hakuna Adhabu.
Kaburi ni kama trash bin/ Dampo la mwili usio na uhai.
Nilitaka kusema hivyo pia, haya maswala ya kupunguziwa adhabu sijui huwa wanayatoa wapi tu. Kwa mukitadha huo, adhabu za Mwenyezi Mungu si za haki. Maana haiwezekani wengine wapate adhabu ya kaburi kuanzia miaka BC huko, afu mwingine aje kuanza hiyo adhabu leo, kesho au miaka kadhaa mbele.

Kifo cha mwanadamu ni sawa na kifo cha wanyama wengine tu, leo hii mbwa akifa mkamuacha ataoza mpaka ageuke mchanga vivyo hivyo kwa binadamu.
 
Demokrasia ilikanyagwa Sana na haki za watu pia.Uimarishaji wa miundombinu ulishamiri Sana kila Kona ya nchi yetu.
 
Kifo cha Lazaro hakikuwa kama cha mbwa uliyemtaja.
 

John Pombe Joseph Magufuli ulikuwa udongo mzuri uliostawi vyema katika ardhi ya Tanzania. Umetenda mema na mabaya,umeishinda vita vingi hadi kuwa Rais ni bahati mbaya umeondoka tukiwa bado tunakuhitaji;tutaendelea kuishi nawe katika Mioyo zetu, tutaendelea kuwa nawe kila siku kwa sala na maombi. Upate raha , upumzike katika udongo mzuri. Msalimie Benjamin W. Mkapa pamoja na Mwl. Julius K. Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…