Zitto Kabwe: Kwaheri John Magufuli, Buriani Tingatinga

Leo anapozikwa kaburini kwake tuzike yale yote yaliyotuumiza pamoja naye.
Its a new day
A new chapter.
Mkuu sijui kama mataga watakuelewa. Wanadhani kuonea kudharau na kuwachukia wengine kutokana na itikadi zao za kisiasa ndiyo maendeleo.
 
Unafiki unafiki unafiki.!
 
Wewe kama una mahaba na mtu wako ni wewe. Hapa panaongelewa uhalisia mahaba pembeni
Kula kulala hajui kinachoendelea mjini ugali unaletwa na Baba
Nyie ndio wale watu wakisikia Mo kutekwa walikuwa wanapiga makofi kisa wivu
 
But, how do you know that there is no peace in his heart?

Ni kipi hasa kinachokufanya udhani kwamba Lissu ana machungu, na hana amani na nafsi yake.

He has not displayed bitterness against what happened to him; unless you expected him to be depressed, regretful and ashamed of what was served to him, as if he begged for it.

Frankly, I do not understand the meaning of these statements you have written here.
 
Tusipofanya hivyo, kuna siku atatokea Rais mwingine atakayeitumia vibaya katiba kuzidi hata akivyofanya Magufuli.
Mkuu, hii inaweza kuonekana kama sio jambo la kuongelea sana, lakini lina maana yake muhimu.

Tanzania itakuwa ni nchi ya bahati mbaya sana kumpata kiongozi mwingine wa aina ya Magufuli (kwa mabaya yake) katika miongo hamsini, kama sio karne nzima.

Nchi hii haina watu wenye tabia za aina yake wengi, kiasi cha kufuatana haraka haraka hivyo.

Hii haina maana kwamba kunahitajika kuwepo katiba mpya, hata kama watakaoongoza nchii hii baada ya Magufuli watakuwa ni malaika.
 
Uko sahihi lakini wapinzani wa chadema wakiongozwa na mjumbe wao asiye na makazi maalumu NDUGU KIGOGO , watakupinga, watakuita msaliti, jitayarishe kwa matuai na majina mengi.

Lakini uko sahihi, wewe na marehemu tofauti zenu zilikuwa siasa.

You are what we call a mature politician.
 
Umeandika mambo mengi mazuri lakini umesahau kukemea nchi yetu kuingizwa kwenye sukumalization,tungemaliza miaka kumi nafikiri kuna baadhi ya taasisi wangekua wanaongea ki sukuma mbele kwani wangekuwa pekeyao ofisi nzima.
All in all pumzika kwa amani hayati!
 
Kumbe na wewe ni CCM tu yaani ugomvi wetu ni CCM sasa kama mnapigiana nao simu mnatusaliti sana CCM imetutesa miaka 50 sasa.
Jitahidi uende kutembelea bungeni na bahati mbaya umeshachelewa nchi ipo kwenye mfumo wa chama kimoja,ukiwakuta wabunge viunga vya bunge wanashirikiana Sana tofauti na unapowaona wanavyosokotana kwa hoja wakiwa ndani ya bunge.
 
MAIGIZO kwa lugha nyingine - UNAFIKI
 
Kaburini hakuna Adhabu.
Kaburi ni kama trash bin/ Dampo la mwili usio na uhai.
Waislam wanaamini adhabu huanzia dunia, kaburini mpaka siku ya hukumu. Itakuwa katumia mtazamo wa dini yake.
 

Rais, umetufunza mengi katika muda ambao umeongoza nchi yetu. Umetufunza umuhimu wa Taasisi katika Jamhuri yetu.

Miaka Sita ya Uongozi wako imetuonyesha kuwa Mtu mmoja anaweza kufanya lolote atakalo bila kujali lolote
Hili funzo ni lazima tulifanyie kazi ili akitokea Kiongozi mwengine kama wewe asiweze kufanya atakalo.




Bila Taifa lenye watu waliostaarabika, wenye upeo na ujuzi, Nchi haiwezi kudumu. Msingi wa Nchi ni Taifa.

Miaka Sita ya Uongozi wako kuna mambo yalitokea Tanzania nisingependa kuyaona yakitokea tena. Watu kupotea hovyo, Wabunge kupigwa risasi hadharani na kutofanyika uchunguzi wowote,

kuvunja vunja misingi ya utumishi wa Umma kwa kuteua Wanasiasa katika madaraka ya Utumishi wa Umma,
kuvuruga Uchaguzi na kuwanyima haki wananchi kuchagua viongozi wanaowataka, raia kunyanganywa pasipoti ,
watu wasio na hatia kubambikiwa kesi na kukaa gerezani miezi mingi kama sio miaka na hali ya watu kuishi kwa hofu. Kwa kuwa naamini haya yote hayatatokea tena Tanzania baada yako, nimekusamehe duniani na akhera, Fi Dunia, Wal’Akhera!
 
Andiko zuri .....lakni hio concept ya kujenga nchi vs taifa ndo sijaifaham uzuri sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…