kanda2,
..mimi na wewe tumebishana sana ktk mijadala mingine lakini ktk hili la kuwashinikiza wabunge kufanya kazi ya kupeleka maendeleo majimboni kwao niko na wewe 100%.
..binafsi mbunge akiendeleza jimbo lake anatusaidia Watanzania wote.
..Zitto akiweza kuhamasisha ujenzi wa shule zenye viwango jimboni kwake ina maana mimi jokaKuu nikitupwa transfer kwenda Kigoma sitakuwa na wasiwasi wanangu watasoma wapi.
..Benki wa wananchi wa Mwanga, iliyoanzishwa kwa juhudi za CD Msuya na wananchi wenzake, ikistawi na kujitanua, Watanzania wote tutaweza kupata mikopo huko.
..kama Zitto atakuwa amejikita ktk masuala ya kitaifa tu, na kusahau kuhamasisha maendeleo jimboni kwake, basi atakuwa amewaangusha wananchi waliomchagua.
Rombo kila kata ina shule za sekondari nne,Mwanga asipofanya Msuya atakuja Maghembe,Daniel Yona.Asha Rose Migiro,Mgonja,Mtoto wa Msuya Mathayo David,Prof Maghembe na wengi sana.
lakini alikotoka Zitto akitoka yeye anaweza kuja mbunge mwingine KANDA2 elimu yake darasa la saba na hana exposure,connection n,k anaweza kuwa na nia nzuri ya kuwaendeleza watu wake lakini hana resource,hana connection nani anamjua wa kumsaidia?
Zitto Kabwe ni kama kasomeshwa na kijiji ili aende kuwakomboa kwa kuwaletea maendeleo watu wake,afanye utaratibu wa kujua NDESAMBURO kafanya nini jimboni kwake Moshi mjini?amepeleka vitu vingi sana,Augustine Mrema ndiye alikuwa msemaji wa issue za kitaifa au kulipua mabomu kama Zitto,lakini pamoja na hayo amefanya mambo mengi ya msingi kwa watu wa jimbo lake kiasi ya kwamba akiomba ubunge anapewa aliwainua kwenye zao la kahawa na kujenga mabarabara.
Ukienda jimbo la Mufindi utaona kazi nzuri ya mbunge wao Mungai,inatakiwa watu wa jimbo la Zitto wawe wa kwanza kunufaida na jasho la mtoto wao,kwani mabomu bungeni wako wengi wa kulipua akimpa Slaa atalilipua,Selelii atalilipua,Anna Kilango analilipua,akilileta hapa JF tutalilipua,lakini asipokwenda kusaidia watu wake jimboni hakuna Mwanajf au Seleli anaweza kwenda kumwakilisha jimboni kwake.
Zinduka Zitto achana na hawa wapambe nuksi wasiokutakia mema wala jimbo lako. Wapemba waliofanikiwa kielimu ni nguvu za Seif Shariff huko nyuma, SEIF aliwahi kuwatengenezea connection ya skolaships kwa watu wake kwenda nje ya nchi kusoma.
waziri mkuu Pinda pamoja na kuwa waziri mkuu wa TAIFA kila kukicha yuko Sumbawanga.