Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya UMMA. Muulizeni kapokea bahasha ngapi na za kiasi gani toka TANESCO, DAWASA, ATC, PPF,.....
Nakumbuka alitaka kuisaidia TANESCO kununua mitambo chakavu ya DOWANS/RICHMOND? Akaona ni heri DAWASCO ifutwe ili ibaki DAWASA ambayo ni mfuko wa nyuma wa suruali za wanasiasa!
JIMBONI KWAKE KAJENGA SHULE NGAPI?MAJI,VITUO VYA AFYA N.K naomba Mwandishi wa Zitto aende jimbo la MKONO au kwa LUKUVI ISMANI-IRINGA.
Haa huo ni ubinafsi kwani lazima mtu ajenge shule au hospitali jimboni kwake?je hamjui Zito kwa uchangiaji wake ameokoa pesa ngapi ambazo amenufaisha taifa zima ili hali huyo Mkono na Lukuvi wananufaisha majimbo yao tu,Watanzania lini tutaacha ubinafsi,nani yuko juu anayetetea masilahi ya taifa na yule anayeangalia jimbo lake tu,kwanza hizo hela za Mkono zina mkono wa ufisadi,kumbuka kesi za benki kuu chini ya rafiki yake Balali kwa siku alikuwa analipwa dola ngapi kutetea uozo.Na je huyo Lukuvi si ni mtu wa mtandao,mbona tunajisahau,ama kweli WATANZANIA NDIO TULIVYO
kwani zito ndio anatakiwa kujenga shule na hela zake za mfukoni????
mkono!!!! hizo hela za bot za kesi za uongo ndio zinakufanya uongeeeee
JIMBONI KWAKE KAJENGA SHULE NGAPI?MAJI,VITUO VYA AFYA N.K naomba Mwandishi wa Zitto aende jimbo la MKONO au kwa LUKUVI ISMANI-IRINGA.
Mimi hizi porojo za Zitto hazina maana kwangu, siku zote mazuri hujitenga, na watu kuyashuhudia sio kumwaga misifa mingi kama robot.Ningekuona wa maana kama ungetoa thatmini ya mafanikio jimboni mwake k.v. mashule, hosipitali, maji, barabara.Wanaotakiwa kuhusishwa na mafanikio directly ni watu wa jimbo lake.huwezi kuanza kutetea watu milion 30 + huku kwako bado kuna matatizo...naomba kuwasilisha hoja
Kazi ya mbunge sio kujenga shule, vituo vya afya etc.
kanda2,
..mimi na wewe tumebishana sana ktk mijadala mingine lakini ktk hili la kuwashinikiza wabunge kufanya kazi ya kupeleka maendeleo majimboni kwao niko na wewe 100%.
..binafsi mbunge akiendeleza jimbo lake anatusaidia Watanzania wote.
..Zitto akiweza kuhamasisha ujenzi wa shule zenye viwango jimboni kwake ina maana mimi jokaKuu nikitupwa transfer kwenda Kigoma sitakuwa na wasiwasi wanangu watasoma wapi.
..Benki wa wananchi wa Mwanga, iliyoanzishwa kwa juhudi za CD Msuya na wananchi wenzake, ikistawi na kujitanua, Watanzania wote tutaweza kupata mikopo huko.
..kama Zitto atakuwa amejikita ktk masuala ya kitaifa tu, na kusahau kuhamasisha maendeleo jimboni kwake, basi atakuwa amewaangusha wananchi waliomchagua.
Mkuu,Mkulu, posho kwa wajumbe wa kamati ni haki yao.Na hiyo Zitto aliiweka wazi kabisa alipokuwa akijitambulisha kwenye mkutano na wakuu wa mashirika yote ya umma.
Na hii lilikuwa echoed na wajumbe wote wa kamati ile na hata mzee mkono alikuwepo kwamba wabunge wanastahili kulipwa posho katika vikao vyao vya kamati na mashirika ya umma na posho hiyo itolewe kwa uwazi (transparently).
Sasa kuchukua posho ya mashirika ya umma si hoja,lete hoja nyingine.
Katika umri wake Zitto ni mmoja kati ya viongozi wazuri sana ambao nchi hii imewahi kujaliwa kuwa nao. Mpangilio wa hoja zake,upana wa uelewa wake wa mambo,bidii ya kujifunza na kuvifahamu vitu ni second to none.
Jamani Zitto yuko kwenye level nyingine,tunapaswa kujifunza kutoka kwa watu wa calibre ile na si kuwabeza kwa kupokea posho ambayo kimsingi imehalalishwa si rushwa ile.
JIMBONI KWAKE KAJENGA SHULE NGAPI?MAJI,VITUO VYA AFYA N.K naomba Mwandishi wa Zitto aende jimbo la MKONO au kwa LUKUVI ISMANI-IRINGA.