ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
UHALALI KISHERIA v UHALALI KISIASA
#NECijiuzulu #INECiingie
Kuanzia keshokutwa tarehe 12 April 2024 Sheria Mpya ya Tume Huru ya Uchaguzi inaanza kutumika kwa mujibu wa GN no. 225 ya 29 Machi, 2024.
Endapo masharti ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024 hakitafuatwa basi, hatutakuwa na tume iliyo ofisini, kwa sababu Tume ni Makamishina na Mwenyekiti wao.
Kujibanza kwenye kifungu cha 27 cha Sheria mpya hakuna mantiki yeyote. Najua wengi, kwa bahati mbaya hata wana mageuzi wa muda mrefu, wamelalia kwenye hoja hii dhaifu kuhalalisha Tume ya sasa kuendelea. Watu wanaowaza hivi wangekuwa Afrika Kusini wangemwacha Mandela afie jela kwa sababu apartheid ilikuwa halali kisheria, lakini apartheid HAIKUWA HAKI wala halali kisiasa.
@TumeYaUchaguzi ya sasa ikibakia ofisini baada ya tarehe 12/4/2024 itakuwapo kisheria lakini HAITAKUWA NA UHALALI WA KISIASA. Mchakato wa uchaguzi ni mchakato wa kisiasa tena wenye misingi ya TRUST.
Tunataka #NECijiuzulu ili #INECiingie
Zitto Kabwe
Mzee mstaafu wa Mwandiga