Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
NIlipata wasaa wa kumsikiliza Zitto kwenye mkutano wa hadhara kwanza wa ACT Wazalendo 2023 pale uwanja wa Zakhem Mbagala.
Niseme kwa kukiri kwamba, kiongozi huyu ambaye ameanzia na kukulia Upinzani ana viwango vyote sahihi vya kuitwa mwanasiasa mwenye hoja. Katika kuunda hoja na kuzijengea misingi yake anatumia msingi wa facts ambazo kwa vyovyote anazitafiti kwanza.
Inawezekana kibinadamu ana mapungufu yake lakini kimantiki na kisiasa yupo mbali sana na wanasiasa wakongwe kama Freeman Mbowe na wengineo. Huyu kijana anaweza kuvaa viatu vya Dkt. Slaa kwenye mizania ya siasa nchini.
Nilikuwa namuona John Mnyika ambaye sasa amepanda na kuwa katibu Mkuu CHADEMA kuweza kuwa na nyota kali ya kisiasa lakini mi ukweli usiopingika namna Zitto Zuberi Kabwe ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuweza kushawishi wasikilizaji kwa mbali sana.
Ni wito wangu wazee waliomzunguka chini ya Mzee Duni Hajji kuendelea kumjenga Zitto ili aweze kujenga jukwaa la wanasiasa mahiri wenye fikra chanya mbadala za kujenga nchi yetu.