GE2025 Zitto Kabwe: Nikiwa Mbunge wanawake watajifungua bure katika Manispaa ya Kigoma

GE2025 Zitto Kabwe: Nikiwa Mbunge wanawake watajifungua bure katika Manispaa ya Kigoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge katika jimbo hilo, Manispaa ya Kigoma itatoa nafasi kwa wanawake kujifungua bure.

Zitto ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 28, wakati wa hafla ya kufunga kampeni zake katika uwanja wa Shule ya Msingi Ujiji ambapo amesema kuwa sekta ya afya inakabiliwa na changamoto kubwa hasa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Endapo nitaibuka mbunge, wanawake watajifungua bure katika Manispaa ya Kigoma, kwani hili ni jambo la msingi katika kuhakikisha afya za mama na mtoto zinabakia kuwa kipaumbele,” amesema Zitto.

 
Back
Top Bottom