GE2025 Zitto Kabwe: Othman anafaa urais Zanzibar anabebwa na rekodi zake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kiongozi mstaafu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mgombea urais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman kwa tiketi ya chama hicho ndiye anayefaa kuongoza kisiwa hicho kutokana na kuwa mstari wa mbele wa kupigania masilahi ya Wazanzibari.

Zitto ameeleza hayo leo Jumamosi Septemba 13, 2025 wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea urais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, maarufu OMO, kwa tiketi ya chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake, Pemba.

“Mimi ni mdogo kwa Othman, sijakutana naye shule wala chuoni au katika kazi za kitalaamu, bali nimemsoma na kumfahamu Othman kwa sababu nilitaka kumfahamu zaidi,” amesema Zitto.

Kwasababu ACT wako sehemu ya Serikali ya Zanzibar, sioni nia yao ya kuchukua kiti cha Urais, toka Maalim Seif aondoke na wanachama wa CUflF kuingia ACT joto la siasa za Zanzibar zimekufa, wachache wako kwenye ulaji.

Kwahiyo ushiriki wa ACT katika uchaguzi Zanzibar ni maigizo tu, na kwa namna ilivyo Othman Masoud ataendelea kuwa makamu kwa mda mrefu sana, hata baada ya Mwinyi kumaliza mda wake 2030.

Aina ya siasa za Zitto toka akiwa Kiongozi wa chama, kimedhoofisha na kuua kabisa upinzani Zanzibar.
 
Back
Top Bottom