Zitto Kabwe, Pemba sio Kigoma

Moja kati ya nyuzi za kijima sana kuwahi kuzisoma humu; hivi hayati Maalimu Seif anaweza kua na ushawishi Kigoma au hata Tabora?

Ieleweke kila mtu ana ngome yake, Maalimu alikua anakubalika Pemba na baadhi ya wana Unguja, hilo wala halina mjadara but the same Maalimu Seif hakua na ushawishi wowote bara; miaka yake yote akiwa katibu mkuu CUF, lini CUF imewahi kupata wabunge wa kuchaguliwa walau 5?

Hao wa term ya mwisho ya Kikwete walipatikana kwasababu ya ushawishi wa Chadema/UKAWA. Sioni ni kwanini umeamua kutengeneza uzi wa kumwambia Zitto kuhusu Zanzibar/Pemba ilihali kijana wa watu ni MUHA wa Kigoma.
 
Najaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
Chuki tu za KIJINGA tu; badala ya kufikiria mbadala wa maalimu Seif mtu anaanzisha tu chuki zake kwa mtu ambaye wala sio Mpemba
 
Najaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
Hata mimi sijamuelewa anataka kumwambia nini Zito?
 
Inaonekana kabisa hamjui siasa na Wala hamfuatilii zbar Kuna mtu anaitwa Jusa Salim,na mwingine Juma khaji duni mnawajua hao? Vichwa Sana kuhusu zito Bado Yuko relini hacha wivu wa kumchimbia shimo wakati kila mtu hatobaki Kama alivyo usimnyooshee zito vidole jinyooshee wewe Kwanza you will not stay forever as you are.
 
Ni mda Sasa vichwa bora kuwai tokea TOKA mfumo wa vyama vingi tz, nazungumzia kutoka chama bora tz CHADEMA, kufanya Jambo makini ili roho za watanzania wenzetu wazanzibar, ziweze kutulia, tafuta vichwa makini TOKA pemba na Zanzibar KWA ujumla mfanye Jambo ili kumuenzi vizuri mh seif (RIP)
 
Upo sahihi kabisa na sasa naiona ACT ile tulio izoea inajirudia kwenye ngozi yake halisi.
Maalim seif akiringia rasilimali watu na hicho ndio kikuu katika mustakbali wa kisiasa kule zanzibar na bara, kama zilitumika dakika 6 wananchi kumfuata ACT kwanini zisitumike ata dakika 10 wananchi kuunga mkono viongozi waliobaki??

Wazanzibar wanahitaji mabadiliko kwa vyovyote iwavyo leo na kesho, usiandikie mate ni suala la muda tu, utajaiyona kasi ya ajabu.
 
Pumzika kwa amani baba yetu,babu yetu mola akupokee katika mwanga wa milele amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…