Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chuki tu za KIJINGA tu; badala ya kufikiria mbadala wa maalimu Seif mtu anaanzisha tu chuki zake kwa mtu ambaye wala sio MpembaNajaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
Hata mimi sijamuelewa anataka kumwambia nini Zito?Najaribu kuwaza kitu gani kimekufanya uandike hii post katikati ya majonzi mengi. Umeshindwa kabisa kuficha chuki yako dhidi ya Zito? kweli mtihani huu.
Na unatakiwa kujua Wapemba sio kondoo kama jamaa zako. Huu ndio mwisho wa janja zako.
ExactlyUpo sahihi kabisa na sasa naiona ACT ile tulio izoea inajirudia kwenye ngozi yake halisi.
PamojaExactly
Hafai kabisaMengineyo.
Tulia 🔪 kiingie kwenye mfupa
Maalim seif akiringia rasilimali watu na hicho ndio kikuu katika mustakbali wa kisiasa kule zanzibar na bara, kama zilitumika dakika 6 wananchi kumfuata ACT kwanini zisitumike ata dakika 10 wananchi kuunga mkono viongozi waliobaki??Upo sahihi kabisa na sasa naiona ACT ile tulio izoea inajirudia kwenye ngozi yake halisi.
Pumzika kwa amani baba yetu,babu yetu mola akupokee katika mwanga wa milele aminaJana tumeshuhudia maziko ya Mwanasiasa mkongwe yaliyofanyika huko Pemba Zanzibar kijijini Nyali Mtambwe na kuona jinsi wananchi wa huko walivyokuwa na simanzi nzito mithili ya kuwa wameondokewa na mfalme wao. Na wengi walionekana kama kuwa sasa ndio basi tena hakuna wa kuja kuwapigania. Maana nilisikia baadhi ya watu wakizuiwa kulia ili wasije kukufuru.
Ni wazi kuwa kwa wapemba Maalim Seif wao walimchukulia kama mkombozi, hata kama angerudi CCM basi Pemba ingerudi kuwa ngome ya CCM.
Sasa ameondoka, hivi kwa akili ya kawaida Zitto anaweza kuwa na ushawishi huko Pemba kiasi cha kutuliza mizuka ya Wapemba?
Pemba tunaiijua tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu wa vyama vingi ni Maalim Seif alikuwa akituliza hasira za Wapemba ambao kwao wanaona kama wanakandamizwa kwa kila namna.
Tusisahau kuwa hata hata baada ya uchaguzi wa 2000 na machafuko makubwa kutokea ni ushawishi wa Maalim uliosababisha kupatikana kwa muafaka wa kisiasa. Hata maridhiano ya kisiasa yaliyopelekea kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar ni sababu Maalim Seif alitumia ushawishi wake kupoza joto Pemba.
Zitto baada ya kuona mambo magumu huku bara ulikuwa unatembelea mgongo wa Maalim Seif huko Pemba. Na unatakiwa kujua Wapemba sio kondoo kama jamaa zako. Huu ndio mwisho wa janja zako.