Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Pigieni kura mgombea mwenye nguvu iwe CHADEMA au ACT-Wazalendo

Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Pigieni kura mgombea mwenye nguvu iwe CHADEMA au ACT-Wazalendo

seedfarm

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
260
Reaction score
2,655
Akiwa mkoani Ruvuma, Manispaa ya Songea mjini akiwahutubia maelfu ya watani zangu wale ambao ukimwachia mke wako dakika mbili ujue imekula kwako Zitto zuberi Kabwe amesisitiza lengo ni kuiondoa CCM madarakani hivyo wananchi wakiona mbunge wa CHADEMA ana nguvu eneo husika apigiwe kura huyo na wakiona wa ACT-Wazalendo ana nguvu apigiwe kura huyo

Akiwasha moto kwa watu wa manispaa ya Songea mjini,Zitto kabwe amesisitiza kuwa watu wa Songea ni watu wa mabadiliko sana ingawa hapo awali nguvu kubwa ilitumika kuzima mabadiliko hayo hapo Songea

Zitto anasema watu wana maisha magumu kila wilaya alizopita yaani wako taabani hawana pesa mifukoni wala hawajui kesho yao

Ikumbukwe muasisi wa Taifa hili na mtu makini kama Rashid Kawawa alitokea Songea,Rashid Mfaume Kawawa alijulikana kama Simba wa vita hii ni kutokana na uongozi wake bora katika vyama vya wafanyakazi enzi za ukoloni

Kawawa aliwatikisa wakoloni na kuwashikisha adabu alipoamua kuhamishia nguvu zake za kuandamana na vurugu bila kuogopa nguvu ya mkoloni kwenye uhuru wa Tanganyika na kumuunga mkono mwalimu Nyerere.
 
Zitto nimekusamehe kwa kazi unayofanya 2020, kwayale yaliyotokea kipindi cha nyuma enzi ukiwa CDM.

Mungu mbaliki Zitto kabwe, pamoja na kamanda Lissu, bila kusahau wanamageuzi wengine.
 
Zitto nimekusamehe kwa kazi unayofanya 2020, kwayale yaliyotokea kipindi cha nyuma enzi ukiwa CDM.

Mungu mbaliki Zitto kabwe, pamoja na kamanda Lissu, bila kusahau wanamageuzi wengine.

..Zitto na Lissu wamekuja kugundua kwamba walikuwa wakichonganishwa na mtu fulani.
 
..Zitto na Lissu wamekuja kugundua kwamba walikuwa wakichonganishwa na mtu fulani.
Hakika mkuu,halafu anachonifurahisha zaidi ananadi sera za CDM katika suala la uraisi. kiukweli Zitto anafanya kazi kubwa, hii combination lazima ma ccm washindwe haraka.
 
Back
Top Bottom