SI KWELI Zitto Kabwe: Polepole si yupo nje ya nchi Canada sasa ametekwaje Tanzania?

SI KWELI Zitto Kabwe: Polepole si yupo nje ya nchi Canada sasa ametekwaje Tanzania?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
"Polepole si yupo nje ya nchi Canada sasa ametekwaje Tanzania?" Ni kweli kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa zamani na mgombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe?

ZItto Okt 7, 2025.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo na ni mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia jimbo la Kigoma Mjini kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, 2025.

Oktoba 6, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa taarifa zikieleza kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ametekwa na watu wasiojulikana hadi kufikia leo Oktoba 7 hakukuwa na taarifa yoyote kuhusu kupatikana kwake.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook wamechapisha grafiki yenye utambulisho wa chombo cha habari cha Mwananchi kikiwa na ujumbe unaodaiwa kuwa ni wa Zitto Kabwe akisema kuwa;

"Polepole si yupo nje ya nchi Canada sasa ametekwaje Tanzania?"

Uhalisia wa Madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo mbalimbali umejirirdhsisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu kama yanavyoonekana katika grafiki hiyo, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na chanzo hicho wala chanzo chochote kingine cha kuaminika.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hakuna chanzo chochote kilichomnukuu Zitto Kabwe kutoa maneno hayo wala yeye mwenyewe kuyachapisha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo X.

Aidha wanaosambaza grafiki hiyo hawaelezi hi wapi haswa na lini Zitto Kabwe aliyazungumza maneno hayo kuhusu sakata la Polepole. Hata hivyo grafiki hiyo inaonekana kuwa ni ya kughushi kutokana na ubora wake kuwa hafifu, kutumia aina tofauti ya mwandiko pia haijachapishwa na chanzo husika.
Back
Top Bottom