Zitto Kabwe: Serikali ilikopa zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge

Zitto Kabwe: Serikali ilikopa zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
ACTWazalendo imesema Deni la Taifa liliongezeka kwa 11% kutoka Tsh. Trilioni 64.5 mwaka 2020/21 hadi kufikia Tsh. Trilioni 71 Juni 30, 2022 ambapo Serikali ilichukua Mikopo kwa 30% zaidi ya idhini ya Bunge.

Vile vile Mikopo ya Nje yenye masharti nafuu iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa 33% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge na kueleza kuwa Serikali imeonesha kutojali na kudharau #MamlakaYaBunge.

Kwa mujibu wa #RipotiYaCAG, bado Serikali ina orodha ya mikataba ya mikopo yenye thamani ya Tsh. Trilioni 1.6 lakini haijapoke fedha za mikataba hiyo, utaratibu ambao umekuwa ikijitokeza kila mwaka na kwa muda mrefu.

===========

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefanya ukaguzi wa Akaunti ya Deni la Taifa na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuboresha usimamizi wa Deni la Taifa. CAG ameeleza kuwa Deni la Serikali hadi tarehe 30 Juni 2022 lilikuwa Shilingi trilioni 71 ambalo ni ongezeko la 11% kutoka Deni la mwaka ulioishia Juni 2021, ikilinganishwa na Sh. Trilioni 64.5 lililoripotiwa mwaka 2020/21.

Uchambuzi wetu unaotokana na Ripoti ya CAG unaonyesha kuwa katika mwaka huu wa ukaguzi Serikali ilichukua mikopo ya ndani kwa 30% Zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano. Vile vile Mikopo ya Nje yenye masharti nafuu iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa 33% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge.

Mwenendo huu unaonyesha Serikali kutojali na kudharau mamlaka ya Bunge. Madhara yake ni kuwa Serikali itabebesha wananchi wake mzigo wa madeni ambao mbele ya safari nchi itashindwa kulipa.

Tunaitaka Serikali iheshimu mamlaka ya Bunge katika maamuzi ya kuchukua mikopo.

Pili, kwa mujibu wa CAG Serikali bado ina orodha ya mikataba ya mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.6 bila kupokea fedha za mikataba hiyo. Hii ni hoja ambayo imekuwa ikijitokeza kila mwaka kwa muda mrefu. Tunaitaka Serikali kufanya mapitio ya mikataba yote ya mikopo ili kufuta mikataba ambayo haitekelezeki na ile inayotekelezeka ipokee fedha na kutekeleza malengo iliyokusudiwa.
 
Waziri wa fedha alisema tujadili maswala ya "waganga wa kienyeji" mambo ya uchumi tumwachie yeye "Dr"!
Natangulia Burundi
 
Zitto tunajua ana chuki na Magufuli ,hivyo lolote lile analozungumza kipindi Cha Magufuli ni chuki tu
 
Back
Top Bottom