Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Niulize swali hili ni kwa wanachama wote wa ACT-wazalendo wenye mawazo mema na taifa hili kama taasisi, hivi ni kweli mnakubaliana na ulaghai wa anakifanya bosi wenu? Yaani vyama vyote vikubwa vya upinzani vinataka mchakato wa katiba mpya lakini Zitto Kabwe anaamini tume huru ya uchaguzi ndio suluhisho la yote, hili kweli wana-ACT mnakubaliana nalo? ACT mnafunga ndoa na CCM kudai tume huru ya uchaguzi badala ya katiba mpya?
Kiongozi makini wa chama cha siasa mwenye mtazamo wa mbali hawezi kufanya anachofanya ndugu Zitto, yaani Zitto kwa maslahi yake binafsi anaungana na CCM kichwa kichwa bila kujua kua wao wanalinda maslahi yao kubaki madarakani? Hivi ukibadili tume ukaacha mfumo mzima wa namna ya kuisikia tume itakusaidia nini? Kwani shida ya madai ya katiba mpya ni Uchaguzi pekee hakuna mengine zaidi? Yaani CCM wao wanadhani wanaodai katiba mpya wote wana shida na ubunge au udiwani na Urais? Shida ya Zitto Kabwe ni ubunge kwa haraka haraka.
Eti na hoja yake dhaifu kwamba tudai tume huru ya uchaguzi ili tupate wabunge wengi wa upinzani ili kwenda kudai katiba mpya, nani kamdanganya kua tume huru ya uchaguzi itakua huru kwa mfumo huu wa katiba iliyopo? Aelezee ni vipi tume inaweza kua huru? Kwa maelezo na taarifa aliyosoma Prof Mkandara ambaye ni kada wa CCM kwa kushirikiana na kina Jaji Mutungi ambaye ni kada wa C CM unafikiri time huru ya uchaguzi itatoka wapi?
Ni vipi utawaondoa. Ma-DED ambao wengi wao ni Makada wa CCM kutosimamia uchaguzi?
Wana-ACT mnalo chaguo la kuendelea na huyu bosi wenu anayewapotosha au kuachana naye kabisa.Mawazo yake ni finyu mno na zaidi anajitazama yeye binafsi kwa maslahi yake na siyo chama.