Pre GE2025 Zitto Kabwe: Sitagombea Urais 2025, nitarejea kuimarisha Bunge

Pre GE2025 Zitto Kabwe: Sitagombea Urais 2025, nitarejea kuimarisha Bunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hana mpango wa Kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 bali anadhani kuna haja ya kwenda kuimarisha Bunge.

Akizungumza kupitia Crown FM, Zitto amesema "Kama unavyofahamu Uchaguzi uliopita wengi tunaamini haukuwa Uchaguzi na ulizalisha Bunge la Chama kimoja, najiona nina wito wa kurejea Bungeni kushirikiana na Wabunge wengine ili kurejesha Siasa za masuala".

View attachment 3086294
hapa zitto kabwe nimemkubari.aende bungeni kujenga hoja .siyo kila mtu anaweza kuwa raisi.
 
Kitaa kigumu. Mitaji imeisha wanarudi bungeni, wewe na ka million moja kako kataisha kabla ya jogoo kuwika.
 
Back
Top Bottom