Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu

Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
Rais Magufuli anasema Kangi Lugola na wenzake wamesaini Mkataba bila ruhusa ya Bunge. Hii ndio standard? Mkataba Gani? Mbona kama hiyo ndio standard wengi hawapaswi kuwepo ofisini hata yeye mwenyewe.

Ujenzi wa Chato Airport Shs 69 bilioni haukupitishwa na BUNGE

Ununuzi wa Helkopta 13 USD 200m za kumlinda yeye Rais haukupitishwa na Bunge

Mkataba wa SGR haukupitishwa na Bunge, Shs 5 Trilioni

Mkataba wa passport mpya haukupitishwa na BUNGE, shs 230 bilioni

Ununuzi wa ndege haukupitishwa na BUNGE, 1.5 Trilioni. Juzi Serikali imesaini Mkataba na Boeing kununua ndege ya pili ya Dreamliner kwa Mkopo ( lease purchase) BILA RUHUSA YA BUNGE wala huo mkopo haumo kwenye mikopo iliyoruhusiwa na BUNGE

Mkataba wa Barrick haukupitishwa na BUNGE

Rais aliidhinisha Fedha Shs 600 bilioni kutoka Benki Kuu ili kununua Korosho zilizoleta hasara ya USD 500m ( Shs 1.2 Trilioni) bila idhini ya Bunge.

Tangu lini Rais anaheshimu Bunge?

Kuna jambo. SIO HILI AMESEMA Rais. Najua kosa la Kangi kafanya Dili kwa kumzunguka Rais. Rais amekasirika. Rafiki yangu Kangi hakujua kuwa hakuna DILI nchini bila mkono wa Rais. Hoja ya BUNGE ni kisingizio tu.
 
Kipimo cha Rais kufukuza watu kwa kusaini mikataba bila ruhusa ya Bunge kinaanzia kwa Kangi ? Yeye Rais @MagufuliJP aliagiza Serikali kununua Korosho kwa Fedha Shs 600 bilioni bila Bunge kupitisha. Hasara kwa Nchi ilikuwa $500m. Rais aliandika barua kujiuzulu?#TUSIDANGANYIKE.

Rais aliagiza Waziri Kabudi na wenzake kusaini Mkataba na Kampuni ya Barrick Gold hapakuwa na kibali cha Bunge wala Mkataba walio INITIAL haujaletwa Bungeni. Mbona hatukumwona Rais akikasirika? #HATUDANGANYIKI.

Mkataba wa kuzalisha Passport mpya ulijadiliwa na TISS na Ikulu na haukuwahi kuletwa Bungeni. Mbona Rais hakuhamaki? #HATUDANGANYIKI

Serikali imenunua Helkopta 13 kutoka Kampuni ya Airbus zenye thamani ya Dola za Marekani 200M bila BUNGE kupitisha Bajeti na wala Mkataba kupitishwa na BUNGE, Rais hajawahi kuonyesha hasira kwa hili. Hii ya Leo ya Zimamoto ina Nini? Ni BUNGE kweli? NOOO. #HATUDANGANYIKI.

Rais aliagiza kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wa Chato wakati hapakuwa na Bajeti iliyopitishwa na Bunge na kazi kutolewa kwa Kampuni ambayo ina mahusiano na Rais na inasemekana ni kampuni yake bila Zabuni yenye ushindani. Kampuni hiyo ni Mayanga Construction Limited #HATUDANGANYIKI.
 
Kweli hata mimi nimejiuliza kidogo,kwanza ni ukweli kuwa sifungamani na Kangi Lugola na Kamishna Andengenye kuhusu huo unaoitwa "ufisadi" wao wa Romania,ila jambo langu mahususi ni kuwa Rais mwenyewe, kama Mkuu wa nchi na Serikali, amefanya mambo mengi bila idhini ya Bunge.

Rais alianza kwa kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vingine na chama chake na makada wa chama chake wakiendelea kufanya mikutano. Katazo hili halipo kisheria na ni uvunjifu wa Katiba aliyoapa kuilinda lakini mpaka sasa Rais haoni kama hilo ni kosa.

Mambo mengi Mh. Rais kayafanya yanayohusisha matumizi ya mamilioni ya pesa bila idhini ya Bunge ambalo ni muwakilishi wa wananchi. Unapokuwa unakemea rushwa, basi si tu ukemee kwa maneno, bali hata matendo yako yaakisi kile unachokitenda.

Hawa kina Lugola sio kwamba walifanya makosa ya kuingia huo mkataba bila kujua, ila walifanya kile ambacho wanaona mkubwa wao anafanya kwa kukiuka taratibu wakajua ndio mtindo wa awamu hii.

What a mother goat does, A child Goat should imitate...
 
Ni kweli. Hata manunuzi ya wabunge wa upinzani pia hayakupitishwa na Bunge.

Watanzania tuache unafiki, tusishangilie hizi double standard.

Ni wazi ubadhirifu na ukiukwaji wa sheria na katiba umetapakaa kila mahali. Waovu ni wengi, muovu mmoja asijione ana haki ya kunyooshea vidole waovu wengine.
 
Asante nimeipenda hii
Rais aliagiza kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wa Chato wakati hapakuwa na Bajeti iliyopitishwa na Bunge na kazi kutolewa kwa Kampuni ambayo ina mahusiano na Rais na inasemekana ni kampuni yake bila Zabuni yenye ushindani. Kampuni hiyo ni Mayanga Construction Limited #HATUDANGANYIKI.
 
Wacha upoyoyo, taratibu zinasema kabla ya pesa za serikali kupelekwa kwenye mradi fulani lazima ziidhinishwe na bunge, kama serikali yake haifuati huo utaratibu na yeye ndie kiongozi wa hiyo serikali unataka alaumiwe Mama Janeth sio?
Bunge gani?
 
Kwani korosho zilikuwa za nani?
Na zilinunuliwa wapi?
Baada ya kununuliwa ziliuzwa na hela kurudi au zilinunuliwa ziwe viburudisho maofisini au?
Mwenye majibu huyo hapo chini.
tapatalk_1577354951190.jpeg


dodge
 
Back
Top Bottom