Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu

Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu

Rais Magufuli anasema Kangi Lugola na wenzake wamesaini Mkataba bila ruhusa ya Bunge. Hii ndio standard? Mkataba Gani? Mbona kama hiyo ndio standard wengi hawapaswi kuwepo ofisini hata yeye mwenyewe.

Ujenzi wa Chato Airport Shs 69 bilioni haukupitishwa na BUNGE

Ununuzi wa Helkopta 13 USD 200m za kumlinda yeye Rais haukupitishwa na Bunge

Mkataba wa SGR haukupitishwa na Bunge, Shs 5 Trilioni

Mkataba wa passport mpya haukupitishwa na BUNGE, shs 230 bilioni

Ununuzi wa ndege haukupitishwa na BUNGE, 1.5 Trilioni. Juzi Serikali imesaini Mkataba na Boeing kununua ndege ya pili ya Dreamliner kwa Mkopo ( lease purchase) BILA RUHUSA YA BUNGE wala huo mkopo haumo kwenye mikopo iliyoruhusiwa na BUNGE

Mkataba wa Barrick haukupitishwa na BUNGE

Rais aliidhinisha Fedha Shs 600 bilioni kutoka Benki Kuu ili kununua Korosho zilizoleta hasara ya USD 500m ( Shs 1.2 Trilioni) bila idhini ya Bunge.

Tangu lini Rais anaheshimu Bunge?

Kuna jambo. SIO HILI AMESEMA Rais. Najua kosa la Kangi kafanya Dili kwa kumzunguka Rais. Rais amekasirika. Rafiki yangu Kangi hakujua kuwa hakuna DILI nchini bila mkono wa Rais. Hoja ya BUNGE ni kisingizio tu.

Baba anavuta bangi.... is okay.

Mtoto anavuta sigara anachapwa bakora.
 
My brother Zitto ni Jambo gani Kiongozi wa Nchi Dr John Pombe Magufuli akifanya/akisema/akiamuru huwa unakubaliana nae???Kila afanyacho Rais ni kosa??umekuwa na ukosoaji wa kijuha Sana kwa muda wote huku ukivumiliwa!!!
Unataka kutuaminisha wewe una akili Sana kuliko wote?
Ni heri uendelee kusoma vitabu tu mwisho wa mwaka utuelekeze umesoma vingapi kuliko kuwa unapayuka payuka Mambo usio kuwa na uwelewa nayo.
 
johnthefool ndio maana umeshindwa kukataa kama wewe sio Mgaya. Kama nasikia harufu ya mkangafu tu. Taasisi gani isiyoheshimu Bunge wala Katiba? Mbona ulanzi unaheshimu mkangafu ambao unaheshimu kimpumu kinachoheshimu pingu? Ukisikia kuzeeka vibaya si kwingine. Futa huo upuuzi wako mwenyewe.
Kipengele gani cha katiba kimevunjwa? Mbona unamawazo ya kushikiwa....
Bunge = Rais + wabunge
Sasa Rais ni mhimili unaojitegemea lakini Bunge ni muunganiko wa Rais na wabunge..ibara ya 62(1) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania..
 
Bila shaka tunaelekea pazuri..
Twende ibara ya 63(1)
Rais kama sehemu moja ya bunge atatekeleza madaraka yote aliokabidhiwa na katiba hii kwa ajili hio...
Ibara hio 63(1) inajibu au inatoa tafsiri ya kifungu cha 3 cha ibara ya 62...hii imewekwa mahususi kwa sbb huenda bunge likagoma kuridhia au hata kutojadili jambo ambalo ni la maamuzi baina ya wabunge na Rais...basi ibara hii inampa Rais ambae ni sehemu ya bunge madaraka yote ya kuamua jambo hilo...
Uliza tena...ujulishwe

Wewe ni muongo sana ,hakuna Ukweli wowote unao endana na haya Maneno yako hapa ktk Kifungu ulicho nielekeza nikakisome.

Kwa Logic ya kawaida tu kama nafasi ya Rais inaweza kuamua na kufanya kila kitu na haipangiwi maana ya kuwa na Bunge ni nini !?

Bunge lipo kwa ajili ya kumsimamia Rais na linaweza pia kumuondoa Rais kwa mujibu wa utaratibu ulio wekwa na Katiba.Mind you Bunge ndio Wananchi wenyewe Mkuu.Pia Rais anaeweza kulivunja Bunge kwa mujibu wa Katiba.
 
Zitto unachosahau, Baba kwenye familia huwa hakosei, na akikosea anazonjia zAke za kumwambia...

Hicho anachokisemA akasome vzr katiba ya nchi,juu ya majukum ya rais kwa manufaa ya Uma..

Sio swala kukiuka kanuni,ila kutekelezA kwa manufaa ya uma...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo hata kama mtu anajenga ikulu kijijini kwake ni sawa tu na pia ni kwa manufaa ya umma.

Kama wewe ni mjinga (Ignorant) jitahidi sana kadri ya uwezo wako kuficha isionekane kwa watu.

Al Bashir alikuwa rais wa Sudan kwa miaka 30 akitawala vizuri tu kwa raha zake na aliingia madarakani kwa mapinduzi na muda woote huo akiwa rais hakuna aliyehoji style aliyotumia kuingia madarakani.

Leo baada ya kubanduliwa kwenye urais wanataka wamfungulie kesi kuwa aliingia madarakani kinyume cha sheria (Katiba). Sasa tafakari, iko siku Rais Magufuli atapata shida sana kwani sheria sio kama Science kwani ni very ambiguous subject without proper formula.
 
Kweli hata mimi nimejiuliza kidogo,kwanza ni ukweli kuwa sifungamani na Kangi Lugola na Kamishna Andengenye kuhusu huo unaoitwa "ufisadi" wao wa Romania,ila jambo langu mahususi ni kuwa Rais mwenyewe, kama Mkuu wa nchi na Serikali, amefanya mambo mengi bila idhini ya Bunge.

Rais alianza kwa kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vingine na chama chake na makada wa chama chake wakiendelea kufanya mikutano. Katazo hili halipo kisheria na ni uvunjifu wa Katiba aliyoapa kuilinda lakini mpaka sasa Rais haoni kama hilo ni kosa.

Mambo mengi Mh. Rais kayafanya yanayohusisha matumizi ya mamilioni ya pesa bila idhini ya Bunge ambalo ni muwakilishi wa wananchi. Unapokuwa unakemea rushwa, basi si tu ukemee kwa maneno, bali hata matendo yako yaakisi kile unachokitenda.

Hawa kina Lugola sio kwamba walifanya makosa ya kuingia huo mkataba bila kujua, ila walifanya kile ambacho wanaona mkubwa wao anafanya kwa kukiuka taratibu wakajua ndio mtindo wa awamu hii.

What a mother goat does, A child Goat should imitate...
Yeye yuko juu ya Sheria na katiba haaaa
 
Zitto anamfananisha Waziri na Rais?.......

Waziri unaweza kumlinganisha na KUB au RC fullstop!
Where's your head bwashee? Go and find where you left then use it! Yaani ccm masalia hujui tofauti ya uliowataja na ukomo wa majukumu yao? Rudi darasani na usione aibu kusoma na wanao!
 
Rais Magufuli anasema Kangi Lugola na wenzake wamesaini Mkataba bila ruhusa ya Bunge. Hii ndio standard? Mkataba Gani? Mbona kama hiyo ndio standard wengi hawapaswi kuwepo ofisini hata yeye mwenyewe.

Ujenzi wa Chato Airport Shs 69 bilioni haukupitishwa na BUNGE

Ununuzi wa Helkopta 13 USD 200m za kumlinda yeye Rais haukupitishwa na Bunge

Mkataba wa SGR haukupitishwa na Bunge, Shs 5 Trilioni

Mkataba wa passport mpya haukupitishwa na BUNGE, shs 230 bilioni

Ununuzi wa ndege haukupitishwa na BUNGE, 1.5 Trilioni. Juzi Serikali imesaini Mkataba na Boeing kununua ndege ya pili ya Dreamliner kwa Mkopo ( lease purchase) BILA RUHUSA YA BUNGE wala huo mkopo haumo kwenye mikopo iliyoruhusiwa na BUNGE

Mkataba wa Barrick haukupitishwa na BUNGE

Rais aliidhinisha Fedha Shs 600 bilioni kutoka Benki Kuu ili kununua Korosho zilizoleta hasara ya USD 500m ( Shs 1.2 Trilioni) bila idhini ya Bunge.

Tangu lini Rais anaheshimu Bunge?

Kuna jambo. SIO HILI AMESEMA Rais. Najua kosa la Kangi kafanya Dili kwa kumzunguka Rais. Rais amekasirika. Rafiki yangu Kangi hakujua kuwa hakuna DILI nchini bila mkono wa Rais. Hoja ya BUNGE ni kisingizio tu.
Ndugu yangu awamu hii uko kijiweni tu! Uliamini siasa ni kazi yako ya maisha, endelea lakini ktk safari hii ya maisha uko taaban. Usihangaishe watu kujadili mambo ambayo yako wazi. Bunge gani hilo ambalo mulizoea kugawana posho mutakavyo? Hakuna uelewa zaidi ya kusoma internet na kuiga mambo ya youtube.
 
Back
Top Bottom