Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Maana ya Muungano itakuwa haipo.Suluhu ni Nchi Moja ,jambo ambalo Wazanzibar hawataki kusikia.
Nyerere alifanya makosa sana,alitakiwa uweke sawa iwe nchi moja toka wakati ule.But hata nchi zilizounganana na kuwa moja,ilitumika force.
pia tunaweza kuboresha kwa kufanya kama ulivyo muundo wa U.K
 
Kaka unatakiwa utafakari kabla hujaongea.
Kama Zanzibar itaendelea mara dufu muungano ukivunjika mbona Pemba tu haijaendelea!?
Nigeria ni nchi yenye reserve kubwa ya mafuta je imeendelea?
Ghana na Senegal nao ni vile vile je wameendelea!?
Zanzibar ni visiwa vinavyokosa watu wenye weledi na wachapakazi.
Ili nchi iendelee inahitaji nguvu kazi yenye weledi na wachapakazi na waliokua foresighted.
Lakini hiko kitu Wazanzibari hawana,nani atawaendeleza!?
Unadhani mafuta yanajichimba tu yenyewe pasi na kuwa na viongozi wenye kuweka sera nyoofu za kiuchumi!?
Nani kakudanganya uchumi wa buluu peke yake unawatosha!?
MADAGASCAR ilijidanganya vivyo hivyo kuwa na uchumi wa buluu na Madagascar ni miongoni mwa mataifa kumi masikini duniani.
Zanzibar muungano ukivunjika hao waarabu wataihama Zanzibar na kuja bara woooteeee.
Zanzibar hakuna room of adjustment mzee.
Kungekuwepo ungewaona kina Ghalib Said na Said Salim Bakhresa wameshawekeza.
Nenda Unguja na Pemba wengi wao watakwambia "NDOTO ZETU NI KUFIKA BARA TUKAFANYE UWEKEZAJI".
Jiulize kwanini wengi wao husema hivyo!?
Investment ni kitu muhimu ila kwa Zanzibar sio sehem rafiki kwa investment.
Msijidanganye Waarabu wenyewe Zanzibar wanaikimbia wanaona matatizo matupu.
Umeongea vizuri sana kuhusu uchumi na nguvu kazi Ya zanzibar utajiri waanchi wala hauitaji majitu yenye misuli mikubwa sana ila inaitaji watu wenye vichwa vizuri kwa mfano Swiden ni nchi ndogo sana ila bajeti yake Tanzani hatuiwezi hata mara 100, Twende hapo Rwanda tu watu wake wanaishi maisha mazuri kuliko Tanzania, Magari ya Rwanda yanayokuja kuchua mizigo bandari ya Dsm na mamia kwa mamia kila siku. Zanzibar kwa idadi ya watu walio nao utalii na Bahari tu vinaendesha hiyo nchi. Sehemu za uwekezaji zanzibar hakuna ila wanaweza wakaendesha uchumi kwa kipato hicho hicho wanachokipata tofauti na sisi. Kuhusu uwezo wa kufanya kazi Wanzanzibar siyo slake kama unavyowaona wanapiga mzigo tu bila shida ila huku kote tumetoka nje ya Mada Mada muhimu muungano uboreshwe ili uwe na tija kila upande. Uu muungano tulionao hauweleweki ni Muungano wa Aina gani ni kama vile ukoloni mamboleo
 

Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mfanyakazi Online Media
Kwa hiyo hoja yake huyu Mhutu Tanganyika ife na Zanzibar iishi?
 
Sasa hapo ndio uneongea nini? Kwanza Huwa mnawapelekea Watangabyika kutawala kule View attachment 2978632
Mwambieni huyo shangazi @fatumakarume kwamba babu yake Abeid Aman Karume alikuwa Mnyasa wa Malawi aliyeenda Zanzibar kutafuta kazi ya ubaharia mwishoe kaangukie kwenye siasa na ndiye aliyekubali kuungana na Tanganyika kwa mapatano na Nyerere na sio kushirikisha wananchi wa pande zote mbili kuridhia.

Karume ni Mnyasa wa Mallawi asijitoe ufahamu eti Ali Hassan Mwinyi kwao Mkuranga,; sawa kwao ni Kisiju na Mwanambaya Mkuranga lakini alienda Zanzibar kusomeshwa ili awe shekhe maalu wa visiwa vya Zanzibar akaangukia kuwa mwalimu wa shule, baada siasa hadi kuwa rais.

Kwani Mkapa si Mmakua wa Mtwara mwenye nasaba za Msumbiji kanda ya Cabo Delgado?

Kwani Kikwete si mkwere aliyechanganya damu na Wadoe na Wamasai wa nchi jirani?

Kwani Magufuli si Msukuma (Kasikazini) wa Butima-Musoma kutoka Bariadi aliyechanganya damu na Wanyambo wa Kagera mpakani na Rwanda?

Kwani Nyerere si Mzanaki wa Butiama-Mara mwenye asili ya Burundi?

Kwani rais aliyepo sasa si Mzanzibar mwenye asili ya Mtwara na Oman?

Kwani Zitto si Mha wa Ujiji Kigoma mwenye asili ya Kalemi Kongo?

Kwani Mbowe si Mchagga wa Hai, Kilimanjaro mwenye nasaba na Wayahudi?

Kwani Shaka si Mzanzibar aliyechanga damu ya Makunduchi na Kilosa, Morogoro?

Kwani imeanza leo Wazanzibar kuweka makazi yao Tanzania bara hasa Kimamba, Kilosa-Morogoro kabla ya mwaka 1967?

Kwani ni uongo kwamba majimbo ya Mwanza mjini hayajawahi kupata wabunge Wasukuma wenye asili ya hapo zaidi ya kutoka nje kama Magu, Kwimba, Bariadi, Ukerewe na Sengerema?

Kwani si kweli kwamba wilaya ya Nzega mkoani Tabora ndio kongwe zaidi ya Singida, Manyara, Katavi, Njombe, Simiyu
 
Umeongea vizuri sana kuhusu uchumi na nguvu kazi Ya zanzibar utajiri waanchi wala hauitaji majitu yenye misuli mikubwa sana ila inaitaji watu wenye vichwa vizuri kwa mfano Swiden ni nchi ndogo sana ila bajeti yake Tanzani hatuiwezi hata mara 100, Twende hapo Rwanda tu watu wake wanaishi maisha mazuri kuliko Tanzania, Magari ya Rwanda yanayokuja kuchua mizigo bandari ya Dsm na mamia kwa mamia kila siku. Zanzibar kwa idadi ya watu walio nao utalii na Bahari tu vinaendesha hiyo nchi. Sehemu za uwekezaji zanzibar hakuna ila wanaweza wakaendesha uchumi kwa kipato hicho hicho wanachokipata tofauti na sisi. Kuhusu uwezo wa kufanya kazi Wanzanzibar siyo slake kama unavyowaona wanapiga mzigo tu bila shida ila huku kote tumetoka nje ya Mada Mada muhimu muungano uboreshwe ili uwe na tija kila upande. Uu muungano tulionao hauweleweki ni Muungano wa Aina gani ni kama vile ukoloni mamboleo
Wala sio nje ya mada vinahusiana.
Maana hiki ulichoeleza ndio sababu ya wao kutaka muungano uvunjike.

Nani kakudanganya Rwanda wanaishi vizuri kuliko Tanzania!?
Miongoni mwa mataifa yenye poor social services Africa Rwanda imo,hata madaktari wao huja Mloganzila na Bugando kufundishwa.
Rwanda ilipoendelea ni Kigali tu,Rwanda is Kigali and Kigali is Rwanda.
Maendeleo hayajawa well distributed huko Rwanda kama Tanzania,Tanzania kila mkoa uendao huduma utazikuta sawa na Dar ila sio Rwanda.

Sweden unazungumzia taifa la watu waliowekeza katika science and technology huwezi fananisha na sisi wala taifa lolote Africa.
Sweden ina wasomi nguli na ni taifa lenye sera nzuri za kiutawala na uchumi.

Zanzibar kusoma hawataki unawezaje kujenga taifa pasi na kuwa na literacy rate!?
Zanzibar kuzalisha wasomi hawataki wao wanashikilia mid man businesses,uvuvi na kuvuna karafuu,unatarajia taifa liendelee kwa staili hiyo!?
Mapato ya utalii peke yake hayatoshi kuendeleza nchi bro usijidanganye.
Madagascar ilifeli vivyo hivyo.
Nchi ili iendelee inahitajika kuwekeza katika sekta tofauti tofauti za uzalishaji.
Uliza wabobezi wa uchumi au hata polieconomists watakwambia.

Mwisho wazanzibari waache kulalamika ilhali muungano unawabeba sana hata katika uwekezaji.
 
Tuseme ukweli, nje ya muungano, SMZ haiwezi kuendesha taifa la Zanzibar hata kwa miezi mitatu.
Muungano kimaisha unatusitiri mnoo wazanzibar.
 
Ndani ya muungano, Zanzibar ni kama kupe tu, tunaishi na kuenenda kwa kudra za mema ya Tanganyika. Siku watanganyika wakitoka usingizini, Zanzibar twafaaa!
 
Zenj wangejitawala wangekuwa mbali sana,wanapiga kazi ila Bara watu Wana mdomo na fitina hatari.

Just imagine licha ya Samia kutoka Zanzibar kuwaokoa kwenye uchumi ulikokuwa unakuta wameishia kumjazia fitina 😁😁
Zenji wanapiga kazi ...umeshaafanya kaz na hao wwtu kweli .kuna siku naamin wwtabaki wemyewe nione miujiza yao .kisingizio cha muungano kuwanyanya hakitakuwepo
 
Tuseme ukweli, nje ya muungano, SMZ haiwezi kuendesha taifa la Zanzibar hata kwa miezi mitatu.
Muungano kimaisha unatusitiri mnoo wazanzibar.
Wajinga na wavivu ndo hujiona kuww mmungano ni kikwwzo cha wao kuendelea
 
Uvivu na ujinga umejaa na kutapakaa Zanzibar kupita maelezo.
Ukiwa mbali unaweza kudhania wazanzibar ni watu kweli kweli, ukikaribia ndio utagundua ni midomo mitupu, maneno matupu, maskini balaa.
 
pesa ndogo sana hiyo,Tena wazanzibar wanatupunja,hiyo ina maana TRA Kila mwezi huchukua billion 33.3🤣🤣🤣,halafu hela hiyohiyo tuwalipe wabunge wao 80 wanaofika huku,wanajeshi,police na uhamiaji walioko kule,wizara zote za muungano na hapohapo wanapata asilimia mbili Tena aisee mbona tunapunjwa sisi wabara
Ndo maana naamini kuna siku huu mungano utavunjika nione watafanya miujiza gani
 
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
Wanasiasa wasaliti na wapumbavu kama hawa....ni hasara kwa taifa...hatuwezi kuendelea
 
Back
Top Bottom