Pre GE2025 Zitto Kabwe: Tume ya sasa ya Uchaguzi (NEC) inapaswa kujiuzulu ili kuruhusu kupatikana kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Pre GE2025 Zitto Kabwe: Tume ya sasa ya Uchaguzi (NEC) inapaswa kujiuzulu ili kuruhusu kupatikana kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao wapya watapatikana kwa sheria gani?
Inashangaza, wabongo uwezo wetu ni mashaka sana. Yaani kubadili jina eti ni jambo la kupongezwa. Zito naye anakuja na kubadili watu, halafu humu anapongezwa. Wakati upatikanaji wa hao watu ni uleule
 

Attachments

  • 20240209_070737.jpg
    20240209_070737.jpg
    29.7 KB · Views: 3
Kiongozi mstaafu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, Tume ya sasa ya Uchaguzi (NEC) inapaswa kujiuzulu ili kuruhusu kupatikana kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa mujibuwa sheria.

Zitto ametuma akaunti yake ya X kuzungumzia suala hilo. Ni saa chache kupita tangu Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mobhare Matinyi kueleza mabadiliko rasmi ya jina la tume ya INEC yataanza Aprili 12, 2024.

Katika ujumbe wake Zitto anasema: “Kuanzia keshokutwa Aprili 12, 2024 Sheria Mpya ya Tume Huru ya Uchaguzi inaanza kutumika kwa mujibu wa GN no. 225 ya 29 Machi, 2024.

“Endapo masharti ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024 hakitafuatwa basi, hatutakuwa na tume iliyo ofisini, kwa sababu Tume ni makamishina na mwenyekiti wao.

“Kujibanza kwenye kifungu cha 27 cha sheria mpya hakuna mantiki yoyote. Najua wengi, kwa bahati mbaya hata wana mageuzi wa muda mrefu, wamelalia kwenye hoja hii dhaifu kuhalalisha Tume ya sasa kuendelea. Watu wanaowaza hivi wangekuwa Afrika Kusini wangemwacha Mandela afie jela kwa sababu apartheid ilikuwa halali kisheria, lakini apartheid haikuwa haki wala halali kisiasa.

"Tume ya Uchaguzi ya sasa ikibakia ofisini baada ya Aprili 12, 2024 itakuwapo kisheria lakini haitakuwa na uhalali wa kisiasa. Mchakato wa uchaguzi ni mchakato wa kisiasa tena wenye misingi ya TRUST.
NENO moja tu kwa Zito ni kuwa ni MSALITI
 
Back
Top Bottom