Ndugu Zitto.
Watanzania walianza kukuita msaliti pale uliposuka mkakati wa kumng'oa Mbowe kutika kwenye uenyekiti wa chama.
Wakati ule tulikuona una uchu wa madaraka na unafanya kazi ya CCM. Lakini baada ya leo kuona anayofanya Mbowe, ya kumsaliti hata mwenyekiti wa chama chake. Mtu aliyekuwa mwambata wake kwa miaka mingi katika siasa za chama. Mtu aliyemsaidia Mbowe kuwasulubu nyie kwenye vikao vya kamati kuu ili kumlinda mwenyekiti.
Najiuliza ni nani msaliti, wewe au Mbowe, ambaye ni mjumbe wa kamati kuu, leo anajumuika na hadhara za CCM.na viongozi wake wakati mwenyekiti wa chama ana kesi ambayo hatima yake anaweza kunyongwa?.
Hivi Mbowe anapata wapi amani kujumuika na watesi ambao lengo lao kuu ni kuia CHADEMA ili watanzania wakose mtetezi?.
Mbowe amegeuka kama mama anayetoa mimba aliyoibeba yeye mwenyewe, au mwanamke aliyezaa mtoto na kisha kumtupa Jalalani. Hivi ndivyo anavyofanya kwa kuisaliti CHADEMA aliyoshiriki kuijenga mpaka leo.
Huenda ndugu Zitto uliona kitu ambacho sisi hatukukijua kwa huyu Mbowe. Na kweli ulipigwa tag ya usaliti na vijana wa Mbowe. Kila ukijaribu kufanya jambo jema wanakuita msaliti, yote hii ili kuzima nyota yako ya kisiasa.
Sisemi kuwa wewe ni mkamilifu, lakini ukilinganisha usaliti wa mageuzi ambao hawa akina Mbowe na wengine wanafanya hasa uzeeni kwa kweli ipo haja ya kukutaka radhi kwa tag ya usaliti uliyopigwa na vijana wa Mbowe.
Sijui nongwa ya Mbowe inatoka wapi, yaani kushindwa uchaguzi na mtu aliyekusapoti kwa miaka 20 ndo iwe nongwa?. Ikufanye utupe mwana na maji ya moto?
Huyu Mbowe ashabambikiwa tuhuma kibao ikiwemo ugaidi, kuuza Ngada n.k. Na wanachadema akiwemo Lissu walimtetea sana. Cha ajabu leo mwenzie anaingizwa ktk tanuri lilelile lakini Mbowe don't care, yaani hajali.
May be hajui jinsi watu walivyompigania alipopigwa kesi ya ugaidi. Watu walikuwa wanafuatilia kesi yake, wengine kupigwa virungu na polisi mahakamani. Leo anawaona watesi ni bora kuliko wenzie ktk struggle
Inauma Sana