Zitto Kabwe: Uzalendo bora ni ule wa kuikosoa Serikali kwa manufaa ya Taifa

Zitto Kabwe: Uzalendo bora ni ule wa kuikosoa Serikali kwa manufaa ya Taifa

Huyu mkongo ni mpuuzi sana. Sidhani kama anatakiwa kuchekewa tena kwa stage aliyofikia sasa.
Akihojiwa na Zuhura Yunus wa BBC nchini Uingereza Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Kabwe amesema uzalendo sio kuitetea serikali bali kulipenda na kulitetea taifa.

Amesisitiza kuwa uzalendo bora ni ule wa kuikosoa serikali kwa manufaa ya taifa na kwamba yeye hajaomba Tanzania ifutiwe mkopo bali mkopo usitishwe hadi andiko litakapoboreshwa ili wanufaika wawe ni wasichana wote bila kujali walipata ujauzito ama la.

Source: BBC Dira ya Dunia

My take: Hii tafsiri ya Uzalendo iliyotolewa na Zitto ni sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sahihi sana maana ameangalia maslahi mapana ua klundi maalum ambalo kwa maoni yangu naweza kuliita about to extinct, zitto ameangalia mbali Sana zaidi ya Kile ambacho wengi wanafikiria maana watoto wa like wanakutana na changamoto nyingi sana kuelekea kuyatafuta maisha yao kwa hiyo wakitengwa kama wadhambi kwa sababu tu wamepata ujauzito itakuwa ni kukiuka maandiko yaliyopo kwenye mkataba
 
Njoo
lumumba kesho nikupe kadi ya ccm. Nauli yako juu yangu
Kwa nini umlipie nauli na sio kumpa maarifa ya kuipata hiyo nauli, hivi ndiyo mnawafanya vijana waone maisha magumu na waendelee kuwa watumwa wa ccm, wakiamini hakuna maisha nje ya ccm.
Ndio maana vijana wanaoingia ccm wakipata maisha hawakai ccm tena, akikaa jua bado ananyonya (wazoea vya kupewa) kuna hatari huko mbeleni ccm kuwa chama cha kuanzia maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao sio wazalendo bali ni wajinga na walinda maslahi. Sasa hivi ndani ya nchi yetu, ni ngumu kutengenisha uzalendo na ujinga.
Mh Selasini wa Chadema juzi kaisifia serikali....... Yeye siyo mzalendo?!
 
Changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike mashuleni, kwanini tusijikite kuboresha hali hiyo isitokee? Badala yake tunataka kuhalalisha uovu???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akihojiwa na Zuhura Yunus wa BBC nchini Uingereza Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Kabwe amesema uzalendo sio kuitetea serikali bali kulipenda na kulitetea taifa.

Amesisitiza kuwa uzalendo bora ni ule wa kuikosoa serikali kwa manufaa ya taifa na kwamba yeye hajaomba Tanzania ifutiwe mkopo bali mkopo usitishwe hadi andiko litakapoboreshwa ili wanufaika wawe ni wasichana wote bila kujali walipata ujauzito ama la.

Source: BBC Dira ya Dunia

My take: Hii tafsiri ya Uzalendo iliyotolewa na Zitto ni sahihi?
Ni sahihi. Serikali huingia, hutoka au hata kutolewa. Serikali inaweza kuwa mbaya au nzuri. Serikali inaweza kuwepo kwaajili ya maslahi ya Taifa au kikundi fulani. LAKINI Jamhuri ni takatifu wakati wote.

Kuitetea Jamhuri siku zote ni uzalendo. Hata kuitetea Serikali ambayo ipo kwaajili ya manufaa/maslahi ya Jamhuri, nao ni uzalendo pia. Lakini pia, kuikosoa au hata kuiondosha Serikali inayotenda kinyume na maslahi ya Jamhuri ni uzalendo pia.
 
Mbona amesalimu amri bwashee?!

Hajazuia mkopo bali ameomba maboresho ya andiko uwe unaelewa na wewe!
Lakini toka mwanzo, kwenye taarifa ya mwanzo ya WB ilisema kuwa Mh. Zito na wanaharakati wa haki za binadamu, wameomba mkopo huo usitishwe mpaka Serikali itakapoweka wazi juu ya sera ya Elimu kwa wanafunzi wasichana wanaopata mimba wakiwa bado masomoni.
 
Kwenye hili Zitto amecheza vizur mana kama zingetolewa wenye makali huenda wangetumia kinyume na malengo ya waliotoa. Lakini tujiulize je baada ya lile tamko la Rais kuhusu watoto kupata mimba je mimba zimeongezeka au zmepunguaa?takwimu zingeletwa hapa ili tuone kama dhamira ilyokusudiwa imefikiwa. Kama la basi Zitto yuko sahihi mana sasa tunakosa vyote!!
Hapa kinachoumiza mtiaji mimba anapga shule tu.halafu msichana anasota nyumbani..!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasaka tonge...hujamuona mwenzio Lugola
Mkuu Ishu ya Lugola imetoa funzo kubwa sana kwa Viongozi wanaojitambua. Kila mmoja atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi na si ktk kumsifu na kumpamba mwenye mamlaka za teuzi. Hata ikitokea umetumbuliwa basi wananchi watakuona kama shujaa wao.
Tizama aibu aliojitia yule Mzee. Hana pakuficha uso wake hasa ndani ya familia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom