Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Viongozi wa Upinzani tulikaa pamoja tukakubaliana kwa Upande wa Urais asimame Tundu Lissu

Aondoe jina kwenye karatasi za kupiga kura, ili wasituibie kura za Lisu kumpa Membe, ili ionekane kashindwa na Membe!

Mbinu hizi sijui kama mnazielewa, utashangaa Membe ana 10% halafu Lisu 6% , Magufuli 80% na mtaambiwa membe alikuwa anakubalika zaidi.
 
Ili aendelee na autocratic system yake ili baadae aongeze muda bila kupingwa.
 
Imeeleweka hiyo, wapiga kura wa sasa sio wajinga. Kura zote kwa LISSU

#NIYEYE
 
Nadhani alishasema kwamba anamuunga mkono Lissu kugombea Urais?
Zitto anajua Lissu ataambulia patupu!!! Anachofanya...ni kumpa coverage ya kutosha Lissu, ili mwisho wa siku Lissu apoke uenyekiti Mbowe na Lissu awe mwenhekiti wa chama. Kisha baadaye Lissu aungane na Zitto ku- merge Chadema na ACT!!

Na wakishafanya hivyo, Zitto ataaanda mpango kamambe wa kukipoka Chama hicho na yeye sasa kuwa Mkuu wa mambo yote, na ataanza kuwadhiaki wote bila kijali juhudi zao za siasa kwenye mipango hiyo!!! Kwa maneno mengine Zitto anataka kurudi Chadema kwa njia nyingine!!!!

Msitoe macho...! Mnashangaaa nini!? Kwani hamumjui Zitto Ha ha haaa!!!! Watani wamechanganyikiwa ....ha haha ahaaa! ( Yote hayo nawaza kipindi hiki.

Ndiyo mambo ya siasa hayo ( Je. Hapa nchini ama nchi nyingine Conspiracy theories ni kosa la jinai!?)
 
Sawa kabisa. Lakini wamechelewa sana. Kwenye uraisi kuna kura zitapotea sana kwenda kwa Membe sababu jina litakuwepo.
Wamechelewa sana hawa kuungana.
Atakae mpigia Membe ni nani na wanachama wa AcT washaambiwa wampigie Lissu?
Labda zihesabike kwake kwa kuiba ili kupunguza za Lissu but vinginevyo sidhani kama atapata kura hata laki moja
 
Hilo jambo ni very tricky kwa sababu:-
1. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Tume wameshachapisha tayari hizo karatasi, na katu hawawezi kutoa hilo jina.

2. Kitakachotangazwa hapa sio KUUNGANA kwa sababu itakuwa ni kinyume na sheria na hatimae kuwapa sababu NEC, na badala yake kitakachotangazwa ni Mgombea X kumuunga mkono Mgombea Y, au chama X kumuunga mkono mgombea wa chama Y!

3. Ili kukabiliana na hicho unachosema, na kama #1 above kimeshafanyika, kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuwaelimisha wananchi kwamba mchagueni "X" kwa niaba ya "Y"

NOTE: Mwaka 2015 nilikuwa na hofu sana kule Pemba kwamba, kwa jinsi walivyozoea Lowassa kwamba ni CCM, jamaa hawatachanganya madesa kweli!! Kilichotokea sote tulishuhudia, Lowassa alimzidi kura Magufuli kule ZNZ!!

Mwaka 2001 CUF walijitoa lakini Seif akawatangazia wafuasi wake kwamba "Wakapige kura za Maruhani"! Na kweli, wafuasi wa CUF walijitokeza kwa wingi mkubwa lakini HAWAKUKOSEA! Kama utakumbuka, ilikuwa kila kura zikihesabiwa, utasikia mgombea X wa CCM amepata kura 112, na zilizoharibika ni kura 7900, kwahiyo Mgombea X anatangazwa rasmi kuwa mbunge!!!

Maana ya hiyo mifano miwili ni nini?!

Wananchi ni waelewa kuliko tunavyodhani! Hofu pekee ni kwamba muda ni mdogo kusambaza ujumbe! Hata hivyo, wanaweza ku-target zile sehemu potential kunakoonekana kuwa na ufuasi mkubwa wa ACT/Membe!
 
Kwani Mgombea haruhusiwi kujitoa ?! Akasema anaona hana ushawishi hivyo kuamua kujitoa?!.

Yote uliyoeleza sawa lakini katafute overall general election results za 2015 utaona, kina Dovutwa na Ahmad Rashid wa ADC hata hawa ACT na Mugwila wao, walipewa kura kwa mtindo wa vote distribution na kumbakizia Magufuli na ccm percentage kubwa hili kuhalalisha ushindi wao.

Kujitoa na kutokuwepo kwenye ballot paper ndio njia sahihi ya kumuunga mkono LISU.
 
Atakae mpigia Membe ni nani na wanachama wa AcT washaambiwa wampigie Lissu?
Labda zihesabike kwake kwa kuiba ili kupunguza za Lissu but vinginevyo sidhani kama atapata kura hata laki moja
Unajua kuna wapiga kura shule hawakuenda na uelewa mdogo pia.
Nakuambia yaani itatokea sana.
Japo na hiyo wizi uliosema kwamba Membe kapewa kura nao yawezekana mia kwa mia asilimia
 
NEC wana hizo taarifa za mgombea mmoja kujitoa?
 
Unajua kuna wapiga kura shule hawakuenda na uelewa mdogo pia.
Nakuambia yaani itatokea sana.
Japo na hiyo wizi uliosema kwamba Membe kapewa kura nao yawezekana mia kwa mia asilimia
Ila naimani zitakuwa chache si za kiasi ambacho hata waliopanga huo mkakati (system) watakazozitegemea.
Mengi yameenda tofauti na mipango yao na hawakujiandaa kwa hali na nguvu na support anayopata Lissu
 
Hivi kuna mahali nchi hii ACT ina ,, ufuasi mkubwa“ ? Na ni wapi huko? Na je ni kigezo gani kinatumika kwa maana nijuavyo mimi act ina Mbunge mmoja tu, sasa huo ufuasi mkubwa mnaouongelea ni upi?
 
Haramu... haitatokea tume kuondoa jina la BM Kwenye karatasi za kura.
Historia ya chaguzi zilizopita inaonesha hivyo.
 
Hiki ndicho utawala huu umefanya "ukabila na udini kwa mbali ila "Uvyama ni Aina ya ubaguzi ulioanzishwa na mamlaka hii na kwa Mara ya kwanza katika historia ya ubaguzi hii ni New Version na itabidi iingizwe na kuzungumziwa kwenye mitaala ya academics na watu wote wajue kwamba utawala huu ndyo innovator wa mfumo huu...Mtake mistake Scholars lazma waandike research kuhusu madhara ya mfumo huu na from there waje na Conclusion!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Haramu... haitatokea tume kuondoa jina la BM Kwenye karatasi za kura.
Historia ya chaguzi zilizopita inaonesha hivyo.
Hivyo hakuna kuungana mkono ni uongo, aachwe Membe afanye kampeni zake huko mtama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…