Aondoe jina kwenye karatasi za kupiga kura, ili wasituibie kura za Lisu kumpa Membe, ili ionekane kashindwa na membe!
Mbinu hizi sijui kama mnazielewa, utashangaa Membe ana 10% halafu Lisu 6% , Magufuli 80% na mtaambiwa membe alikuwa anakubalika zaidi.
Hilo jambo ni very tricky kwa sababu:-
1. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Tume wameshachapisha tayari hizo karatasi, na katu hawawezi kutoa hilo jina.
2. Kitakachotangazwa hapa sio KUUNGANA kwa sababu itakuwa ni kinyume na sheria na hatimae kuwapa sababu NEC, na badala yake kitakachotangazwa ni Mgombea X kumuunga mkono Mgombea Y, au chama X kumuunga mkono mgombea wa chama Y!
3. Ili kukabiliana na hicho unachosema, na kama #1 above kimeshafanyika, kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuwaelimisha wananchi kwamba mchagueni "X" kwa niaba ya "Y"
NOTE: Mwaka 2015 nilikuwa na hofu sana kule Pemba kwamba, kwa jinsi walivyozoea Lowassa kwamba ni CCM, jamaa hawatachanganya madesa kweli!! Kilichotokea sote tulishuhudia, Lowassa alimzidi kura Magufuli kule ZNZ!!
Mwaka 2001 CUF walijitoa lakini Seif akawatangazia wafuasi wake kwamba "Wakapige kura za Maruhani"! Na kweli, wafuasi wa CUF walijitokeza kwa wingi mkubwa lakini HAWAKUKOSEA! Kama utakumbuka, ilikuwa kila kura zikihesabiwa, utasikia mgombea X wa CCM amepata kura 112, na zilizoharibika ni kura 7900, kwahiyo Mgombea X anatangazwa rasmi kuwa mbunge!!!
Maana ya hiyo mifano miwili ni nini?!
Wananchi ni waelewa kuliko tunavyodhani! Hofu pekee ni kwamba muda ni mdogo kusambaza ujumbe! Hata hivyo, wanaweza ku-target zile sehemu potential kunakoonekana kuwa na ufuasi mkubwa wa ACT/Membe!