Zitto Kabwe: Wabunge hatujaamua kuwa serious

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
263
Reaction score
16
Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alisema kwa kosa hilo alilofanya Waziri ambalo ni la kudharau maazimio ya Bunge, wabunge wangeweza kuamua apelekwe gereza la Keko kwa siku saba.

``Alichokifanya Mheshimiwa kama tukiamua kuwa `serious` (makini), angekwenda Keko siku saba,`` alisema Kabwe huku akinukuu sheria ya madaraka na wajibu wa Bunge ya mwaka 1988.

Habari zaidi: Mzindakaya arejea upya,ampiga kombora Waziri


.....ndiyohiyo
 
Hili ndilo bunge letu na hawa ndio wabunge wetu.
Kongoli story ya 'Bunge Butu' kwenye google muone jinsi Bunge la Tanzania linavyoitwa Bunge Butu.
Kama Mhe. Waziri Mkuu anawaambia wananchi wachukue sheria mkononi, halafu anamwaga chozi bungeni, then its over and its ok. Unategemea nini kwa mawaziri wake?.
Mhe. Zito, tunajua kuna baadhi yenu mko serious but no matter how serious you might be, at which majority?. Nothing.
 
Hili ndilo bunge letu na hawa ndio wabunge wetu.
Kongoli story ya 'Bunge Butu' kwenye google muone jinsi Bunge la Tanzania linavyoitwa Bunge Butu.

PASCO,
Unapoliita bunge letu BUTU,
Unalinganisha na bunge gani?
 
PASCO,
Unapoliita bunge letu BUTU,
Unalinganisha na bunge gani?

Nadhani hili ndo mojawapo la bunge la vilaza ktk dunia hii, believe me my man!! Ukitoa akina Zito, Slaa, Kilango, Mwakyembe, etc waliobaki ni maguluguja tu! Yaani hakuna pa kulifananisha, njaa inaua watu pale bungeni, hakuna lingine!!
 
Naomba kusaidia hapa, anamaanisha bunge lenu!! jeezy!! Bunge lenu la TANZANIA ni butu!! get it into your head!

KILLMINATI,
Kama umeamua kusaidia, saidia kabisa.
Unalinganisha bunge la Tanzania na bunge gani ndipo useme kwamba ni BUTU?
 
Nadhani hili ndo mojawapo la bunge la vilaza ktk dunia hii, believe me my man!! Ukitoa akina Zito, Slaa, Kilango, Mwakyembe, etc waliobaki ni maguluguja tu! Yaani hakuna pa kulifananisha, njaa inaua watu pale bungeni, hakuna lingine!!
USITOE HAO, kwani wao wapo nje?
 
PASCO,
Unapoliita bunge letu BUTU,
Unalinganisha na bunge gani?

Sio lazima ulinganishe na bunge lolote lile ili kusema bunge la Tanzania ni "BUTU" Kwani kwamano ukiambiwa panga ni butu ni lazima uulize ni butu kama la nani? Kwani panga ama kisu butu havijulikani?

Bunge halifanyi yale waliyotumwa kufanya na wananchi na umasikini unaongezeka na ufisadi...Huo ndio ubutu wenyewe huo...Mikataba mibovu inasainiwa wao wanapiga meza tu.

Nadhani utakuwa umepata mwanga kidogo ndugu Makyao.
 
- Sisi wengine siku hizi tunali-appreciate bunge letu maana kama sasa mpaka Waziri Mkuu analazimishwa kuomba radhi, wakuu tumetoka mbali sana na hili bunge, I mean wanahitaji heshima japo kidogo!
 
kwani Mkuu JK anasemaje?
au hatakiwi kuongea kitu?
tanzanians we're unblvble....
things we do, the way we react,
 
- Sisi wengine siku hizi tunali-appreciate bunge letu maana kama sasa mpaka Waziri Mkuu analazimishwa kuomba radhi, wakuu tumetoka mbali sana na hili bunge, I mean wanahitaji heshima japo kidogo!

Mkuu naungana na wewe, tumepiga hatua. Nadhani tangu tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi wabunge wetu wengi ni kama walikuwa wameoza, maslahi ya chama na viongozi wanachama yalikuwa mbele kuliko maslahi ya taifa. Sasa hivi at least kuna harufu ya bipartisan na tripartisaniship kujaribu kulinda maslahi ya taifa, bunge linaonesha dalili ya kuondoa status ya kuwa mhuri wa serilkali. Wabunge lazima wasifiwe kwa hilo, sasa hivi hawalolomi tu bungeni, at least wanawashikisha adabu watu wa executive. Kuna wakati nilikuwa naoa media yetu ambayo bado iko ill informed(kuna few exeptions) ina nguvu kiasi kuliko hata bunge. sasa hivi uhai upo.
Lakini hata hivyo bado old school politics zinaendelea, ni ajabu kuona mtu anakubali kosa mbele ya bunge halafu wabunge wanapiga makofi this is very funny. Kuna aina fulani ya kumlinda mtu kwa sababu yeye ni mwanaCCM au kwa kuwa yeye ni member wa executive, hata kama anafanya ujinga ulio wazi. Ndio maana mheshimiwa Kabwe anasema wabunge hawako serious, bunge lina uwezo mkubwa kuliko linavyoonesha na linavyobehave.
Wenzetu Kenya wako a bit more serious, ndio maana hata nchi yao iko hatua 10 mbele kuliko Tanzania.
 
mfano ni bunge la Botswana, mwaka juzi waziri wa elimu aliomba fungu la bajeti na ilipofika next bajeti akaja na report kwamba katumia fedha na baadhi zimebaki ajazitumia, wabunge walimkomalia kwamba aliomba fedha kwa kazi maalum na kwa kurudisha kwake fedha ina maana ajatimiza malengo aliyoombea fedha, nakwambia asubuhi akuwa tena waziri.
 
angeanza yeye kutoa hoja na yeye aache uzushi !!!!si mbunge pia
kama ni bogus na yeye yumo,,wameshamtuliza niini kijana zamani alikuwa machachari kweli mambo kama haya anayanyanyukia si mchezo lakini sasa hivi duh!!!
hongera zito kwa kusoma nyakati!!!
 
Uyo Zito wameshamwekea ulaji sasa japo ananguruma hapo bungeni lakini wahusika hawana tena wasiwasi nae,juu ya vitisho vya wabunge utawasikia wakitutumka sana unaweza kusema watakamatwa,kumbe hamna kitu,sijawahi kusikia hoja binafsi kuwekwa na wabunge wa upinzani au kuweka shilingi ,nasikia kuna shilingi,sasa hawa wabunge wa upinzani kwa nini wasidai katiba Mpya kwa kuweka hiyo shilingi yukaona nguvu yake, naamini CCM wanaweza kuweka na kuna yule mbunge wao amesema atawasilisha hoja Binafsi ili Mkwere aendelee kuongoza kwa miaka kumi mingine na hiyo hoja naona itapita tu.
 
naamini CCM wanaweza kuweka na kuna yule mbunge wao amesema atawasilisha hoja Binafsi ili Mkwere aendelee kuongoza kwa miaka kumi mingine na hiyo hoja naona itapita tu.
ITAPITA NA MATULU YAO!!!WAJARIBU WAONE
 
``Alichokifanya Mheshimiwa kama tukiamua kuwa `serious` (makini), angekwenda Keko siku saba,`` alisema Kabwe huku akinukuu sheria ya madaraka na wajibu wa Bunge ya mwaka 1988.

Huu ni ukiukwaji wa makusudi kabisa wa sheria za Bunge na sidhani kama ni jambo ambalo linatakiwa lisichukuliwe seriously. Kama sheria za Bunge zipo na zinaonyesha wazi kila adhabu ambayo mbunge anastahili kuipewa kwa kufanya kosa fulani- kwanini zisifuatwe? Tumeona jinsi ambavyo sheria ilichukua mkondo wake kwa Zitto, tena huku ikiwa imepindwa- why not for her? Sasa itakuwa kila waziri akijishtukia kachemsha anakimbilia kuomba radhi tu coz they know it works and they will get away with it!
 
mkuu kana -ka -nsungu ni hivi bado huyo zitto hana haki ya kulalamika au kupiga kelele wakati ye yumo ndani habari kama hizi alitakiwa aongee mrema,,lipumba,,kama alikuwa anaona sheria zinapindishwa na anauhakika sheria ilishawahi kufwata mkondo wake juu yake why not her??then kwa nini asimwambie spika???kama ulimsikia namnukuu

mh spika kosa alilofanya ni kubwa kwa kuufuata sheria hata uwaziri angetakiwa avuliwe
"""""""""""""LAKINI NAOMBA TUSIFIKE UKO"""Why???mbona kwake walimfikia tena si uko
mpaka barabarani wakaendelea kudili nae !!!!ashukuru mungu wazee wa kigoma!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…