BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kiongozi wa ACT WAZALENDO, Zitto Kabwe alikuwa kwenye kipindi cha Tv ndani ya Clouds TV asubuhi ya leo Aprili 11, 2022 amezungumza mambo mengi ya kisiasa, haya ni baadhi ya yale aliyozungumza kwenye interview yake hiyo:
Amesema mazingira ya kisiasa Nchini Tanzania yamebadilika na kuna uhuru sasa hivi.
“Watu wako huru kuzungumza hawaogopi chochote kama kutekwa, kushtakiwa na tutumie hii nafasi ya uhuru kuzungumza tukae kama viongozi tuzungumze..
“Inawezekana kama viongozi tuna tofauti zetu za kibinafsi au kivyama, inatakiwa hizo tofauti uziweke pembeni na kuikabili changamoto iliyopo mbele na tuitumie hii nafasi vizuri,” Zitto.
KUHUSU TUME HURU YA UCHAGUZI
"Tuweke mazingira ambayo tume itakuwa huru na kuna mazingira ambao unaweza kubadilisha baadhi ya vifungu vya katiba. Mimi sio mpenzi sana wa kuweka viraka kwenye katiba nisigependa tuifumue katiba.
KUHUSU KATIBA MPYA
“Nisingependa tuifumue katiba wakati tunakwenda kwenye katiba mpya yenyewe hasa kwa bunge hili ambalo tunalo sasa hivi ambao 97% ya wabunge wanatoka chama kimoja."
Source: Clouds TV