Pre GE2025 Zitto: Kama Dkt. Mpango aliitwa Mrundi nani wa Kigoma atapona?

Pre GE2025 Zitto: Kama Dkt. Mpango aliitwa Mrundi nani wa Kigoma atapona?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mpaka tar 27 mambo yatakuwa motooo!

====


Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameibua kumbukumbu za harakati zake za kutetea maslahi ya mkoa wa Kigoma na viongozi wake, akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Nyamsanze, kata ya Buhoro, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Ijumaa, Novemba 22, 2024.

Katika hotuba yake, Zitto amekumbushia jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kumtetea Dkt. Mpango alipokumbwa na madai ya kutokuwa raia wa Tanzania, licha ya yeye kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Hata Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, alivyoteuliwa kuwa Makamu wa Rais, kuna watu wajinga waliosema yeye si raia wa Tanzania, wakasema ni Mrundi. Hakuna mtu wa CCM aliyejitokeza kumtetea, wakati yeye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chao. Mimi nilisimama nikasema, sawa, huyu ni CCM, lakini ni mtu wa Kigoma. Kama anaambiwa si raia, mtu gani wa Kigoma atapona?" Amehoji Zitto.

Zitto ameongeza kuwa harakati zake za kutetea maslahi ya Kigoma hazijawahi kuzingatia mipaka ya majimbo, akisisitiza kuwa alikuwa sauti ya wananchi wote wa mkoa huo, bila kujali anatoka jimbo gani.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

"Mimi tangu nimechaguliwa kuwa mbunge mwaka 2005 mpaka nilivyoondolewa bungeni mwaka 2020, nimefanya kazi kubwa sana ya kuwatetea na kuwasemea. Nimetetea Kigoma bila kujali jimbo ambalo nipo. Nimetetea Kagerankanda wakati mimi si mbunge wa Kasulu Vijijini, nimetetea kule Uvinza mimi si mbunge wa Kigoma Kusini, nimetetea kila mahala.", ameeleza Zitto.

Zitto ametumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa kata ya Buhoro na wilaya ya Kasulu kwa ujumla kuwachagua wagombea wa ACT Wazalendo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024. Amesema kuwa chama hicho kinaendelea kushikilia ajenda ya kulinda maslahi ya wananchi wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla, lakini ni muhimu kuwa na viongozi wa ngazi za chini watakaoshirikiana naye kuimarisha harakati hizo.

"Nimekuwa mbunge nikiwa kijana mdogo wa miaka 29. Sasa hivi nimeoa, nina watoto, ninazeeka. Ninahitaji wasaidizi. Chagueni wagombea wa ACT ili tushirikiane kutetea maslahi ya Kigoma."
 
Back
Top Bottom