Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Huyu jamaa mi ananiachaga hoi sana. Si angetaja ha wawili basi. Hivi kuna watu wanamuamini huyu mti
 
MsemajiUkweli

Mmoja wa hao watu ni Yusuph Manji!!! Badala ya kumpa kesi ya uhujumu uchumi, kuhatarisha usalama wa taifa, na utumiaji wa dawa za kulevya... alikumbwa na hatia ipi miongoni mwa hizo?!

Mtakana sana, lakini serikali hii wakati mwingine huwa inafanya mambo kwa kukomoa raia wake!!! Ni kutokana na ukweli huo, ndo maana wengi wanaokuwa target ni lazima wapewe kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji pesa kwa sababu ni kesi zisizo na dhamana!!

Lengo ni kuwakomoa wahusika kwamba lazima wakae ndani!!

Na kweli, wengi wanakaa ndani lakini mwisho wa siku, majority wanakutwa kutokuwa na hatia na mashitaka mazito kama hayo... but who cares! Mission Accomplished! WASHAKOMOLEWA TAYARI!!

Aidha ni juzi tu hapa Evans Aveva na Godfrey Nyange (Kaburu) wamefutiwa mashitaka ya utakatishaji wa fedha huku wakiwa wamekaa mahabusu kwa miezi kadhaa!!

Turudi kwa akina Rugemarila!! Kama lengo sio kuwakomoa kwanini walioshirikiana nao kuchota pesa za Escrow bado wanadunda mtaani?!

Ruge na Singasinga hawakutumia mitutu na vifaru kwenda kuchukua pesa za Escrow bali walipata baraka zote za viongozi waandamizi pamoja na mahakama!! Kwanini basi wawekwe ndani peke yao lakini miezi kadhaa baadae waambie waombe radhi na kutoa pesa ili waachie!!!

Mtu kama Singasinga ambae amedhohofika kweli kweli, hata kama hana hatia, unadhani ataacha kuomba radhi?!

Anyway, endeleeni tu kutetea lakini ukweli utabaki pale pale.
Naona ukweli ulio wazi kabisa hasa hapo kwa Ruge na Singa Singa maana hela za escrow zilipata hadi idhini ya bodi ya wakurugenzi wa TANESCO pamoja na waziri Muhongo akiwa Nishati!!!!!!!!!!!!!!!
 
Siwajui wengine. Wale wa Acacia, akitoa maagizo alisema, 'wananishtaki mimi! Kamata maofisa wao wakuu wote, tuone kama hawatakuja kwenye meza ya mazungumzo'
Duuh unanikumbusha rafiki yangu Deo Mwanyika na Asa Mwaipopo.
 
Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Basi waachwe wasipewe msamaha, watashinda kesi na serikali itakosa hela na itawalipa fidia
 
Nadhani unapobambikiwa kesi.. anayetakiwa kutoa ushahidi usio na shaka ni yule anaekubambika hiyo kesi ili kuishawishi mahakama. Hivyo aliye kwenye nafasi nzuri zaidi mahakamani ni yule mbambikiwa kwa kuonyesha hahusiki kwa namna yoyote ile. Lakini leo inaonekana kampuni X ilijipatia fedha isivyo halali, mmiliki wa kampuni hiyo ni wewe na nyaraka zote zinaonyesha ulichukua hiyo hela . Halafu useme huhusiki umeonewa.

Kutoa tamko la jumla hivi kwamba kila mhujumu uchumi kabimbikiwa kesi ni uhuni wa kisiasa. Wananchi wamelalamika sana huko nyuma kuhusu ufisadi. Wanasiasa wamepiga kelele sana including mwanasiasa uchwara, Zitto. Sasa hatua zimechukuliwa wanageuka kuwatetea walewale mafisadi.

Hebu tujiulize ni Mpinzani gani wa kisiasa wa magufuli aliebambikiwa kesi ya uhujumu uchumi. Halafu tujiulize tena hizo fedha ziliibwa au hazikuibwa? Na zikirudishwa zinamnufaisha nani ? Magu au taifa kwa ujumla. Acheni chuki, unafiki na ushabiki wa kipumbavu.
Hogwash
 



Zitto atakuwa amepata ‘amnesia’ sio bure ni juzi tu hapa alisifia maamuzi ya watu hao hao kukamatwa akiitaka serikari iende mbali zaidi.
 
Mfano mtu katuhumiwa kwa kosa moja au mawili cha ajabu watengeneza kesi wanamjazia kesi za kujibu 400 au hata zaidi ukizisoma kesi zenyewe hazina tofauti zaidi ya kubadili sentesi tu, utitiri wa kesi unatumika vibaya kuwachanganya watuhumiwa, na je?wale wanaotumika kuwabambikia kesi wao watachukuliwa hatua gani? Kumtesa mtu miaka 4 mwingine ni masikini kama Michael Wambura atarudisha pesa ipi? akaotoe wapi?au wauze nyumba zao?

Lengo la kuwekwa ndani ili ufilisike kabisa na familia yako isambaratike kabisa kwa kutokuwepo kwako.
 
Utawala huu wanaweza hata kuwabambikia kesi familia yako yote pia wakavhukua mali ulizowaachia cha msingi ni kuomba mungu waache hii Dhambi ya kuwabambikia watu kesi kienyeji kwa njia haramu

Kagame ndie master mind copy na paste kuwakomoa na kuwaporra watu Pesa baada ya kushuka kwa vyanzo vya mapato.
 



Zitto atakuwa amepata ‘amnesia’ sio bure ni juzi tu hapa alisifia maamuzi ya watu hao hao kukamatwa akiitaka serikari iende mbali zaidi.


Kutenda haki ni kutafuta ushahidi uliokamilika kisha wawahukumu kama sheria isemavo.Na sio kuwakamata watu kwanza kisha ndo utafutwe ushahidi hii ni kinyume na jamii iloyostaarabika
 



Zitto atakuwa amepata ‘amnesia’ sio bure ni juzi tu hapa alisifia maamuzi ya watu hao hao kukamatwa akiitaka serikari iende mbali zaidi.
Wanamjua walisha sema ndumila kuwili ni uthibitisho tu wa undumila huo
 
Huwa nayakumbuka maneno ya Baba wa taifa. "Katiba ya Tanzania imempa madaraka makubwa sana Rais wa Tanzania. Siku akiingia madarakani mwendawazimu, tutapata shida". Hayo ni maneno ya Nyerere. Nitawaletea video clip, ninayo.
Hahahaaah aisee
 
Tatizo siyo katiba, ni watu wanaokubaliana na hali hiyo huku wakilalamikia maandishi.
Kwani katiba iliyopo haijawahi kuvunjwa?
Uwepo wa katiba (maandishi) ni jambo moja na watekelezaji (watu) ni jingine.
Bila watu wanaojielewa na majasiri, makubaliano ya kimaandishi hayana uzito wowote.


Hao watu Wa kujielewa watoke wapi hali wameuwa elimu nzuri aliyotuachia mkoloni iliyopelekea watu kujitambua.Hawa wamewekeza kwenye ujinga na umasikin kama mtaji Wa kutufanya watakavo.Leo waliokuwa waandimizi Wa dikteta boutlafrica Wa algeria wanachezea mvua uenda kizazi kijacho kitarevenge
 
This is so obvious .....!!

Kama DPP. PCCB na DCI wanashindwa kuwatengenezea mashitaka watuhumiwa kwa miaka mitatu hapo unategemea nini!!?
Huwezi pata ushahidi kwenye kesi za kubambika ndo maana wanashindwa kuwapeleka mahakamani wakashindane kwa hoja mbele ya sheria .Kukwepa aibu ya kushindwa wamekuja na hili la kuwalamisha waombe msamaha.
 
Hawa watu watakuja ipa serikali ijayo hasara ikitoka hii wataisthaki serikali iwalipe fidia hapa ni kodi zetu ndizo zitatumika.
 
wengi wao ni wale waliosemwa na wapinzani kuwa ni mafisadi...
leo wanatetewa na haohao wapinzani...

Ni wakati mzuri wa kuwatetea na akina Seth na Rugemalila/Lugemalila......japo tuliwaita mafisadi before
Alietoa rushwa na aliepokea rushwa wote inabidi wachukuliwe hatua, iweje sasa kina Ngeleja na wenzake kina Joka la makengeza wanadunda mtaani? Na kama kweli hawa ni wahujumu uchumi sasa mbona uchunguzi haukamiliki miaka mi4 yote? Wamefukunyua huko wakaona hakuna dalili ya kushinda kesi ndio wamekuja na gia nyingine ya nipe nikupe.

Watz tuna akili nyie wa huko lumumba endeleeni kuwa misukule
 
Upelelezi unaendelea miaka3 hadi 4 hii sio sawa .Hata kesi zenye prima-facie evidence unasema bado upelelezi unaendelea? hapo kuna mashaka.

No makosa kumshikilia mtuhumiwa kisha ndo uanze kutafuta ushahidi ni kinyume na haki za binadamu.Kama ushahidi aujakamilika kwann wakamate watu.Halafu tuna watunza sheria mahakimu,majaji,wapelelezi tena ni wasomi na nyumba za ibada wanakwenda huwa najiuliza huwa wanakwenda kufanya nn nyumba za ibada hali wameshikilia uhuru na haki za watu.
 
Back
Top Bottom