Zitto kuwa mgeni rasmi show ya Mwana FA, huku Sugu akiwa kwa Jide

Zitto kuwa mgeni rasmi show ya Mwana FA, huku Sugu akiwa kwa Jide

Status
Not open for further replies.
Presha ya show kubwa za magwiji wa muziki hapa nchini MWANA FA "The Finest" na lady jay dee" miaka 13 ya jide" imezidi kupanda baada ya show hizo kutawaliwa na wanasiasa, Zitto alisema yeye atakuwa kwa mwana FA, huku mbunge kijana aka kinega sugu akichagua kwenda kwa Jide aka ANACONDA aka binti machozi kutoa full sapoti

Mwana FA atapiga nyimbo zake zote Live akiwa na bendi kongwe na bendi maarufu hapa nchini ya WANANJENJE!
HONGERA KWA HAWA WASANII KWA HATUA WALIYOPIGA........................

Duh! hapo Mh Zitto amechemsha Huyu Mwana FA niliemwona kwenye Bango la kampeni la kuchangia ccm? Kwanini huyu Mh. Zitto anashindwa Kujitambua? kwanini ? Watu husema akikua ataacha! sa atakua lini huyu?
 
Zitto ni blank kabisa mambo ya bongo flavor so hajui kitu na sio kosa lake

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Joto-Hasira.., Yahaya n.k., Lady JD the Anaconda Queen Wa muziki wa bongofleva Tz.
 
Na nyie nao...kwani kuna mshindani ya kisiasa? acheni hizo? kama ZZK amealikwa asiende? labda wangeandika huku kwa fatuma ni CCM ama kwa jide ni CHADEMA, Jide mwenyewe hajatangaza kama yeye ni CHADEMA naona shabiki wana viherehere
 
Katika dunia ya leo usithubutu kupambana na mwanamke, wewe mwanaume utashindwa tu, katika janga hili ruge and co mtaumia zaidi, sympathy aliyotengeneza jide itawahukumu hadi kaburini. Dunia ya leo wanawake ni very powerful , ndivyo ilivyo, wao ni wazazi, ni walezi, na wengi sasa wamethubutu mfumo dume hauna nafasi, wanaume tujifunze kuto under rate nguvu za wanawake.

Phd ( safarini QUBEC)
 
Zitto kabwe ni sawa na wala haishangazi kwani inajulikana ni ndumi la kuwili na msaliti tu kama Mwanafatuma,ndege wa rangi moja huruka tundu moja!!

Hivi nyinyi wafuasi wa cdm kwanini akili zenu mgando sana?hivi nilazima watu wote washabikie kitu kimoja?toeni upuuzi wenu hapa wakati jide clouds wanamrusha kila sec mbona wenzake hawajalalamika kama yeye?
 
zitto siku nyingi yupo kundi la wasaliti ,dunia nzima ilishamtoa kwenye kundi la wapambanaji..

Hata mimi namshangaa huyu Zitto, yaani uwezo wake wa kupambana kibabavichaabavichaa upo chiniiiiii..

Wenzake wakisimama bungeni hawajengi hoja, wanaporomosha matusi mazito mazito kwa viongozi wa chama tawala na serikali yao lakini yeye sijui yupo mrengo gani..

Utamkuta anaongea na "maadui" huku ametabasamu badala ya kununa,nadhani hayo malezi yenye maadili aliyopata ndio yamemuelemea.

Aondoke atuachie genge..ups sorry chadomo letu.
 
Inawezekana zitto hajui mchezo unao chezwa. lakini wanasiasa wana maujanja ya kufa mtu. anaweza mtuma mtu amuakirishe kuepusha soo. mia
 
Katika dunia ya leo usithubutu kupambana na mwanamke, wewe mwanaume utashindwa tu, katika janga hili ruge and co mtaumia zaidi, sympathy aliyotengeneza jide itawahukumu hadi kaburini. Dunia ya leo wanawake ni very powerful , ndivyo ilivyo, wao ni wazazi, ni walezi, na wengi sasa wamethubutu mfumo dume hauna nafasi, wanaume tujifunze kuto under rate nguvu za wanawake.

Phd ( safarini QUBEC)

Una maana gani tusipambane na mwanamke ?

Kuna manufaa gani ya kuwa na mwanamke asiyetoa kipaumbele kwenye kuitafuta suluhu na kuendekeza ugomvi.

Bila kujali mwenye kosa ni yeye au Ruge Jide anastahili hukumu yake na sio kuonewa huruma kwa jambo la kijinga.

Wasifu namba moja wa mama ni kuilinda na kuitetea amani, kutafuta suluhu, kuonyesha upendo n.k, na sio anavyofanya Dada kwa kujiunga na makundi ili kuhakikisha amani haipatikani.

Tunamtofautisha vipi yeye na maelfu ya wanawake wanaofanya vitendo vya ukatili haswa kwa watoto wa kambo au wasichana wa kazi majumbani, wanawachoma moto, kuwanyima chakula na mateso ya kila aina, ukatili wa aina hii unatokana zaidi na roho mbaya za visasi ambazo kwa bahati mbaya kina mama zimewakamata.

Kwa hiyo tukikuta mama kamvunja mtoto wa kambo mkono kumkomoa mumewe anayemsaliti tumuunge mkono ?

Ahurumiwe tu pale inapostahili na sio kumpa kichwa na kumuita commando ili atimize haja yake ya kulipiza kisasi

Kama mwanamke acheze part yake.
 
Kama anavyotumika Mwanafa kwa kupewa uraisi wa TFU na kina rugay,kuahidiwa atapewa ubunge wa Muheza kupitia CCM,kupewa ubalozi na usemaji wa FISTULA ili hali yeye si mwanamke na wala sio daktari( kwa akili yako amepewa ubalozi wa fistula kwa vigezo vipi yeye,linah,barnaba na kina mwasiti??!!))))

Teteeni dhulma na upumbavu lakini hatutaacha kuwaambia ukweli,cha ajabu hamtetei wala kukanusha tuhuma za clouds kujaza watangazaji mashoga!!!

muheza hapati kitu! Tupo vijana tumesimama hatutaki mbururaz, kama mwanafatuma
 
Presha ya show kubwa za magwiji wa muziki hapa nchini MWANA FA "The Finest" na lady jay dee" miaka 13 ya jide" imezidi kupanda baada ya show hizo kutawaliwa na wanasiasa, Zitto alisema yeye atakuwa kwa mwana FA, huku mbunge kijana aka kinega sugu akichagua kwenda kwa Jide aka ANACONDA aka binti machozi kutoa full sapoti

Mwana FA atapiga nyimbo zake zote Live akiwa na bendi kongwe na bendi maarufu hapa nchini ya WANANJENJE!
HONGERA KWA HAWA WASANII KWA HATUA WALIYOPIGA........................
Naona hapo ni mtifuano wa Sugu na Zitto
 
si unajua muziki sikuizi unaambatana na itikadi za siasa kwa hiyo kila mtu ana demopkrasia ya kuamua ajiunge na sera za nani teheee hiyo ndo tanzania bana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom