Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!

Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!


Hata walio mabingwa wa lugha huanza kufanya makosa ya kitoto ikiwa wanaishi kwenye jamii inayoharibu au isiyojali usanifu wa lugha kwenye uandishi au mazungumzo. Maana humo, watasikiliza na kusoma makosa ya kitoto kila mara.
Nilifundishwa na mwalimu mwingereza aliyeishi kwa miaka 16 Scandinavia, siku moja alikiri kwamba kiingereza chake kimekuwa hovyo kwa sababu niliyoeleza hapo juu.
Naam! Mfano wako upo juu ya mstari!
 
Hiki ndo kinachotakiwa, watanzania tunapenda sana kusifiwa hata kama tumeboranga, enzi za U good boy or good girl, doing a fantastic and excellence job wakati huna lolote zimepitwa na wakati, ukikosea unaambiwa "Mbwa anapigiwa kwenye tukio" ni lazima tujenge utaratibu wa kukosolewa ndiyo tutajenga taifa lenye uajibikaji na siyo taifa la ndiyo Mzee.BIG UP MR:ZITO.
Ladies and gentlemen, we have to be very serious na hao wabunge,we're the one who employed them even though wakifika mjengoni wanatugeuka tena mgeuko mkubwa wa nyuzi 180. Tusiwe na ushabiki wa kivyama, tuangalie zaidi maslahi ya Taifa then chama.
I believe that together we can make it.
 
Kwani lazima Zitto agombee jimbo la Ubungo ndiyo wewe ugombee? Basi wewe haujaweka maslahi ya taifa mbele bali unataka tu kuonekana kuwa umemshinda Zitto. Maneno mengi sana nyuma ya ID ya JF mkuu kama unaweza kagombee usimsubirie Zitto.

Jamani ee! Wengine wakienda maliwato wanakuwa na kiu, hamuoni wana makopo mawili mawili? wasiwape shida hao.

Hoja hapa ni kama Sumari majibu yake yalikuwa ya hovyo hovyo au la! sisi wendawazimu tunasema yalikuwa ya hovyo hovyo, nyie wenye akili pungufu mnasemaje??
 
Jamani ee! Wengine wakienda maliwato wanakuwa na kiu, hamuoni wana makopo mawili mawili? wasiwape shida hao.

Hoja hapa ni kama Sumari majibu yake yalikuwa ya hovyo hovyo au la! sisi wendawazimu tunasema yalikuwa ya hovyo hovyo, nyie wenye akili pungufu mnasemaje??
Hii ni post ya wiki. Big up na hao uliowauliza wanasemaje hawatatokeza kujibu😀 maana wanajitokeza kujibu simple questions😀
 
sijui walitaka mh. Zitto atumie msamiati gani zaidi ya neno OVYO kama wanaompinga walivyo ovyo
 
NILIPENDA sana kushiriki mijadala ya kisiasa na kiuchumi inayoendelea nchini walau kila wiki. Lakini kwa bahati mbaya, wiki iliyopita sikufanikiwa kufanya hivyo kutokana na majukumu ya kisiasa yaliyonilazimu kuelekea nyumbani Kigoma.

Moja ya majukumu yangu katika maandalizi ya jimbo jirani na lile la Kabwe Zitto, kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo Inshalaah, Mungu akijalia nitahitajika kutoa mchango wangu wa jasho, machozi na damu kuhakikisha nchi yetu inazidi kujinyofoa kutoka katika mikono ya shetani ya ukiritimba wa chama kimoja cha siasa.

Ni kwa sababu hiyo nilishindwa kuchangia wiki iliyopita. Ni bahati mbaya kwamba katika taifa lisilo na mwelekeo kama letu, mikanganyiko ni mingi kiasi kwamba ni vigumu kujadiliana kwa kina jambo moja, kabla mkanganyiko mwingine haujaibuka.
Naam! Hizo ndizo sifa za taifa linaloyumba. Taifa lenye mitikisiko kwa kukosa mwelekeo. Taifa lenye ombwe la uongozi.

Siku za usoni nitajadili hili la ombwe la uongozi lakini kwa kufanya tathmini ya kwanini kiongozi aliyebahatika kuwa na nguvu ya umma kama Jakaya Kikwete wa mwaka 2005 ameshindwa kufanya mabadiliko ya msingi japo kuweza kugusa hisia za baadhi ya matarajio ya matumaini ya jamii ya Watanzania, jamii yenye kiu ya uongozi kwa miongo mingi sasa.

Katika mwendelezo wa mijadala ya misukosuko ya kisiasa inayoendelea kulikumba taifa letu, nimepata kujadili mwenendo wa Bunge letu la bajeti, katika wiki mbili zilizopita nilijadili maelekezo ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuhusu ahadi yake ya kuchukua hatua kali dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kwa madai ya kukaidi amri ya kiti.

Zitto, alisema majibu yaliyotolewa na serikali kwa Dk. Wilibrod Slaa, alipotaka taarifa za ufisadi wa Meremeta, yalikuwa ya hovyo hovyo.

Nakumbuka niliandika: “Spika Sitta usiturejeshe zama za Buzwagi.” Zama ambazo alijishushia heshima yake kwa umma kwa kiasi kikubwa baada ya kuamua kujisahau na kusimamia Bunge kwa staili ya kusimamia vikao vya CCM.

Msingi wa makala yangu ile ilikuwa ni kumkumbusha Spika Sitta kwamba anapaswa kujua kuwa yeye ni Spika wa Bunge katika mfumo wa vyama vingi, na ili kujijengea heshima anapaswa kuwa mvumilivu na kuepuka kufanya maamuzi yanayoweza kurahisisha mtu kumtazama kwa sura ya mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, bali kwa sura ya Spika wa Bunge mwenye msimamo wa kati, asiyeyumbishwa na maagizo ya vikao rasmi wala vya siri ndani ya CCM.

Ni kwa msingi huo, pengine nimshukuru Spika Sitta japo kwa tahadhari kwa uamuzi alioufanya kuhusu hukumu hiyo dhidi ya Zitto, kwamba baada ya kutafakari, amebaini kuwa Zitto hakuwa na kosa wala hakuvunja kanuni yoyote kwa kusema: “Mh. waziri alitoa majibu ya hovyo hovyo.”

Hongera Spika kwa kukubaliana na hoja ya Zitto, ambayo msingi wake ni hoja ya Dk. Slaa kwamba majibu ya serikali kuhusu Meremeta yalikuwa na bado ni ya hovyo hovyo.

Nimesema nampongeza Spika kwa tahadhari kwa sababu kubwa moja, kwamba ingawa anakubaliana na Zitto, kuwa hakuvunja kanuni yoyote kwa kusema waziri alitoa majibu ya hovyo hovyo, lakini wakati huo huo anasisitiza kuwa Zitto alipaswa kutii amri ya kiti.

Sasa amri ya kiti ni nini? Amri ya kiti ilimtaka Zitto kufuta kauli yake kwamba waziri alitoa majibu ya hovyo hovyo kwa Dk. Slaa ndipo aendelee kuchangia.

Amri ya Zitto, alikataa akiamini kauli yake haivunji kanuni. Lakini Spika anaunga mkono hoja gani? Spika anaunga mkono hoja kwamba kauli ya Zitto kwamba waziri alitoa majibu ya hovyo hovyo si kinyume cha kanuni yoyote.

Sasa hapa kuna utata. Amri ya kiti siku ile chini ya Zuber Ally Maulid, ilitokana na hoja kwamba kauli ya Zitto ilikuwa ni uvunjifu wa kanuni. Sasa kama Spika anakiri kwamba kauli ile haikuvunja kanuni yoyote tofauti na ilivyoelezwa awali na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge siku ile.

Inakuwaje Spika tena aagize Zitto kumwomba radhi Maulid aliyekuwa mwenyekiti wa kikao siku hiyo? Je, kwanini Spika Sitta hajaweka wazi kuwa msimamo wa Mwenyekiti wa Bunge siku ile, kuwa kauli ya Zitto ilikuwa uvunjifu wa kanuni si sahihi?

Kama si sahihi, ni adhabu gani anayochukuliwa mwenyekiti huyo kwa kutoa hukumu isiyo sahihi? Kwa nini Zitto aombe radhi kwa kukaidi amri ya kiti ambayo Spika ameonyesha wazi kuwa haikuwa amri sahihi? Zitto aombe radhi kwa kosa lipi? La kutokuheshimu amri isiyo sahihi ya kiti?

Ninasema hayo kwa sababu kwa msomaji yeyote anayefanya tafakuri ya kina, atakubaliana na mimi kwamba mgogoro huu msingi wake ni kuyumba kwa msimamo wa aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge siku ile.

Maana itakumbukwa kuwa baada ya Zitto kutakiwa kwa mwongozo wa Spika kufuta kauli yake, kwamba alitoa kauli ya kuudhi, mwenyekiti alisema “…Ok, Mheshimiwa Zitto naomba uendelee kuchangia lakini bila kurudia neno ‘majibu ya hovyo hovyo,” lakini baada ya wabunge wa CCM kuzomea na kupiga kelele kwamba “afute! afute!” Mwenyekiti wa Bunge aligeuka na kusema:

“Naomba msikilize kwanza nimalizie, Zitto futa kwanza kauli yako, kisha uendelee kuchangia tafadhali.” Hapa ndipo msingi wa kosa ulipo.

Ndiyo maana ninasema, katika hili tatizo si kwamba Zitto ni jeuri kwa kukataa kutii amri ya kiti, tatizo kiti kiliyumba. Sasa kiti kinapoyumba kanuni zinasemaje?

Je, ni halali kwa mbunge kutii kiti hata kinapoyumba? Nadhani tukio hili litufundishe kwamba kuna haja ya kuboresha kidogo kanuni za Bunge ili kuangalia haki ya mbunge kiti kinapoyumba.

Nasema hivyo kwa sababu ni vigumu mbunge kukiri kosa na kuomba radhi kwa kiti ilhali mazingira yanaonyesha wazi kuwa hana kosa eti tu kwa kusubiri kukata rufaa baadaye.

Kwa nini wabunge wasikubaliane kwamba mbunge ambaye hakubaliani na kiti aruhusiwe kuendelea kuchangia lakini aelezwe kwamba hatua zitachukuliwa baadaye dhidi yake badala ya kuondolewa kwenye kikao ili pawepo na nafasi kwanza ya mjadala husika kutofunikwa na mjadala mwingine, lakini pili ili kutoa nafasi kwa mbunge kutochukuliwa hatua ya kukigomea kiti kabla hoja ya kiti kupimwa na kuangaliwa kama ilikuwa hoja sahihi?


Kwa mfano, kama ingekuwa inaruhusiwa kwa mbunge kupingana na kiti, kuachiwa aendelee kujadili kwa ahadi kwamba suala husika litaamuliwa baadaye, Zitto asingelazimika kumwomba radhi mwenyekiti, wala Spika Sitta asingeweza kumkalipia na kumtoa nje Mbunge wa Bariadi, kwani baada ya mjadala kikao cha kujadili kosa la Zitto kingebaini wazi kwamba mbunge huyo hakufanya kosa dhidi ya kiti.

Bali kiti ndicho kilifanya kosa kumlazimisha Zitto afute kauli yake kwa madai kuwa kauli husika inavunja kanuni kumbe si kweli kama alivyobainisha Spika Sitta.

Ninachokisema hapa ni kutafuta fursa ya mbunge kuchukuliwa hatua baada ya kuthibitika kwamba ana kosa, kuchukuliwa hatua au kulazimika kufuta kauli baada ya kuthibitika kwamba kweli ana kosa na si tu kiti kinaposema mbunge futa kauli, basi mbunge analazimika kwanza kufuta.

Chukulia mfano, uamuzi aliouchukuliwa na kiti, siku hiyo chini ya Spika Sitta kwamba Mbunge wa Bariadi, John Cheyo atolewe nje kwa sababu hakubaliani na majibu ya serikali…ni wazi kwamba maamuzi haya ya kiti chini ya Spika Sitta, hayakuwa sahihi pengine ndiyo sababu kumekuwepo na taarifa kwamba Spika amemuomba radhi Cheyo kwenye kikao cha kamati ya uongozi.

Huo ni uamuzi mzuri, lakini Kama Spika Sitta analazimisha Zitto aombe radhi ndani ya Bunge kwa kinachoitwa kosa la kukaidi amri ya kiti, kwamba lazima iwe ndani ya Bunge, kwa kuwa kosa limefanyika humo, kwa nini kosa lake (Spika Sitta) la kumkaripia mzee mwenzake Cheyo, hata kumwondoa nje ya kikao, adhabu yake isiwe kuomba radhi ndani ya Bunge kwa kuwa kosa lilifanyika humo?

Kweli Spika Sitta, amejitahidi kuruka mitego na kutafuna mfupa aliorushiwa na Zitto, wasiwasi wangu ni kwamba mfupa uliorushwa na mzee Cheyo pengine unaelekea kumkwama.

Kwani wananchi tunasubiri kujua hatima ya udhalilishaji mkubwa aliofanyiwa Cheyo, hatima yake nini! Haitoshi kuomba radhi kwenye kamati ya uongozi lhali umma ulioshuhudia udhalilishaji huo dhidi ya mzee mapesa, tukibaki gizani. Kanuni ni msumeno Spika, ikila kwa wabunge lazima siku nyingine ile kwako.
 
Back
Top Bottom