Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Mi nadhani kufananisha makosa ya Chief Mangungo na makosa tunayoyafanya kizazi hiki ni kumkosea adabu chief huyo.

Kwa kipindi kile angeweza kupata wapi kujua thamani ya kioo, shanga na vitu vingine....! Lakini sisi kila kitu kwa sasa kinajulikana lakini tunachokifanya hakika hata mangungo angejinyonga kwa kujilaumu kwa alichokifanya.

Ni bahati mbaya kabisa Tanzania haijawahi kupata kiongozi mzalendo wa kweli kwa sababu jamii kwa ukubwa wake imekuwa "corrupt" hivyo ni wachache mno wenye kujali maslahi ya Taifa. Wengi hata tunaoibua madhaifu na ufisadi ni kwa ajili ya kujijenga kisiasa tu akishashika nafasi tunabaki kushangaa alivyobadilika.

Mkubwa, mimi nadhani ili tuanze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo sharti la kwanza kabisa ni kuviondoa na kuvifuta kabisa vyama hivi vya kisiasa vilivyopigania Uhuru....

Mimi naamini tatizo liko hapo kwa sababu kwa jinsi mambo yalivyo hata umlete nani kuwa kiongozi chini ya mifumo ya vyama hivi kuongoza taifa letu......

Nakuambia atakuja na nguvu za gesi ya soda ya Coca Cola mwisho anauvaa mfumo huu wa kihayawani, naye anakuwa walewale na kulainika kama mkate kwenye chai ya maziwa......

Tena huyu (John Pombe) pamoja na kulazimisha asifiwe hata na mawe nadhani ndiye atakuwa the worst ever president taifa la Tanzania kuwahi kuwa naye....!!

Kwa hili alilolileta Zitto Kabwe, kama ni kweli hata kwa 10%, basi linathibitisha haya niyasemayo....

Kwa sababu haiwezekani kwa mihemko tu Rais wa nchi bila hats kujipa muda was kutafakari mambo ktk engo zote unaamka na kuja na National and International Televised speech dhidi ya watu wa nchi yako na dunia kwa ujumla kuwa umekamata investor mwizi ktk sekta ya madini ktk nchi yako wa $190bn, ukafunga shughuli zake, na kuwaaminisha watu kuwa tutalipwa......!!

Lakini eti, mwisho wa siku mnaishia kuingia makubaliano ya kipuuzi na kishenzi kama haya na badala ya yeye kuilipa nchi, nchi ndiyo inamlipa MTU kama huyu ulichokuwa unakidai na at same time unampa na migodi ya madini yote!!

I predict kuwa huyu bwana ndiye Rais atakayeingia kwenye rekodi ya marais wezi na matajiri kuliko wote. kuwahi kutokea tangu uhuru.....!!

Hakuna namna nyingine unayoweza kuitafsiri hii situation iwapo tu kilicholetwa hapa na mbunge huyu ni KWELI na HAKIKA...

Naamini huu kamwe hauwezi kuwa ni uzushi kwa sbb kama haya makubaliano yamewekwa wazi huko kwenye masoko ya hisa UK na NYSE, basi maana yake ishu hii ni hakika na ni ukweli mtupu na kuwa ndivyo ilivyo!!
 
Naona hii imekuwa yamoto kwa wazee wa kusifia kila kitu siwaoni humu waje na fact na kujibu hoja za msingi hata bro wetu p mayalla nae katoka nduki du awamu hii tutashuhudia mengi sana
 
Utasikia mimi nalinda Mali za nchi. Uzuri hakuna mtu ninaye mwamini ndani ya CCM
 
Zito huo no ujinga kwani kama unge yasema hayo kabla ya hili sekeseke kufika note huku ungepata hasara gani.?
Sasa unaongea sahizi tuta kusaidiaje?
Auwewe unafurahi tukikosea we we ukosoe uonekane Wa maana sisi tupate hasara tuwe tayari tumeliwa!.nimekudharau kuanzia Leo!
 
Wale maprofessa uchwara/njaa walisema makinikia yana thamani mara kumi zaidi ya ile Acacia iliyorekodi. Usafirashaji wa makinikia utakaporuhusiwa utaona thamani inayoandikwa ni ile ya Acacia (sasa Barrick) na si ya maprofessa uchwara.

Maprofessa uchwara/njaa walisema Acacia haina uhalali kisheria Tanzania lakini ili Barrick aweze kuingia makubaliano na Serikali inampasa amalizane na Acacia.

Na bado wakasema smelter inaweza kujengwa hapa Tanzania. Watu TMAA wamefukuzwa kazi kuonekana wezi. Hii yoyote ni kwa sababu Rais Magufuli alipewa anachotaka kusikia.

Leo hakuna smelter imejengwa. Kodi ya $190 bilioni hakuna. Na Acacia (sasa Barrick) itaendelea na shughuli zake. Mwisho wa siku tunaonekana tulikuwa tunataka tu pesa bila kuwa na ushahidi wowote wa kuibiwa.

Ni kiasi gani cha investor confidence kimeshuka kwa sababu ya mgogoro huu? Huu si uhujumu uchumi?

Hawa maprofessa njaa/uchwara wametufanya watanzania wote tuonekane wapuuzi duniani. Hawa maprofessa njaa/uchwara wangekua hata na aibu kidogo wangeomba msamaha kwa upuuzi wao walioaminisha watanzania.

Mtu anaendeshwa na hisia zake anaenda kuharibu biashara za watu bila kujali akiamini anaisaidia nchi huku anashangiliwa na washamba wenzake.
 
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
Pascal Mayalla njoo ujibu
 
Kwa jambo hili Zitto unataka kutuambia kama bunge mna sauti gani, waonaje basi ukalipeleka bungeni ili serikali iwajibike kwa kuvunja sheria mliyoitunga.
Tofautisha BONGE na BUNGE now tuna BONGE not Bunge
 
Mpinzani wa kupinga. Yeye (Zito) awamu ya nne ndiye alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa kinana ni mwizi mkuu wa rasilimali za taifa. Kuwa ni jangiri maarufu wa meno ya tembo. Ajabu hivi sasa yeye ndiye mtetezi mkubwa wa Kinana. Hivi huyu binadamu ni binadamu wa aina gani?
Umeelewa alichoandika?
 
Zitto mwaga upupu baba, hata ile ndege ulisema ya mtumba na ukaweka na vielelezo, sasa hivi ndio inaruka kutoka Mumbai...
 
Taarifa isiyo na uthibitisho itabaki kati ya kweli na uongo. Nasubiri upande wa pili wathibitishe, ili niijue aina ya viongozi tulionao nchi hii.
 
Serikali yetu sheria nyingi inazitunga kwa mihemko na kuzipitisha kwa dharura...

Ndio maana baada ya muda kidogo sheria zilezile zinarudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho ama serikali yenyewe inazivunja.

Tuache kutunga sheria kwa ajili ya mtu ama kampuni fulani.
Inapendeza kuona 'objectivity' inarudi mahali pake.
 
Back
Top Bottom