Andiko ni zuri, ila hatujui ukweli uko wapi kiuhalisia, kwa sababu ni taarifa ya upande mmoja.
Kungekuwa na taratibu za kupata majibu kutoka upande wa pili, upande wa akina Kabudi ingekuwa ni jambo jema sana, lakini sote tunajuwa hilo hapa kwetu haliwezekani.
Hata hivyo, kuna mambo muhimu kayagusia ndugu Zitto, kwa mfano hiyo asili mia 16 ambayo hutufunika macho wengi wetu.
Lakini inaumiza zaidi, inapofikia mahala mambo kama hili hapa chini kutopewa nafasi na watu ambao ni zao la moja kwa moja la juhudi za waasisi wa nchi hii. Hawa akina Kabudi, ndio walikuwa wakisemwa kwamba ni vijana wanaotumwa kwenda kuhemea ili kuiondoa nchi yao kwenye jamga la njaa.
Hawa ndio waliopewa vibaba vya mwisho ghalani ili waje wakalijenge taifa lao!
Ona sasa jambo kama hili hapa chini ambalo ni vigumu kutoamini yaliyoandikwa hapa.
Mimi nadhani inalazimu tujaribu utaratibu walionao nchi kama China. Watu wanaokosa uzalendo kama hawa wasipewe nafasi ya kuchezea maisha ya waTanzania.