Zitto - Msimamo wake kuhusu katiba mpya

Zitto - Msimamo wake kuhusu katiba mpya

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
21,859
Reaction score
19,736
Katiba ni mwafaka wa kitaifa. Kitendo cha CCM kuweka msimamo wa Serikali mbili kwenye muundo wa Muungano kinaua kabisa maana ya kuwepo na mjadala. 'Caucus' za vyama kwenye kazi nyeti kama ya kuandika katiba ya nchi iwe marufuku. Kuna kundi lina lengo la kuzuia katiba Mpya kupatikana. Kwa vyovyote vile lazima tuwashinde wapinga mabadiliko hawa kwa kuunganisha nguvu za wananchi. Tusirudi nyuma "Forward ever, Backward never" - Nkrumah

Source FB profile yake(ofisi ndogo)

My take;

kiongozi muadilifu na mwanamapinduzi ya kweli huitaji torch kumtambua. Angalizo langu binafsi pia kitapokuja kipengere cha kujadili muungano na muundo wake msisahau kujadili ubaguzi/muungano wa WAPEMBA NA WAUNGUJA muda ukifika mtaelewa what i mean
 
zitto hana jipya swala la katiba ccm ndo wameshavuruga ndo maana wamejaza wajumbe wa ccm lakini mm nasema ccm kifo chao kimeshakaribia
 
Katiba ni mwafaka wa kitaifa. Kitendo cha CCM kuweka msimamo wa Serikali mbili kwenye muundo wa Muungano kinaua kabisa maana ya kuwepo na mjadala. 'Caucus' za vyama kwenye kazi nyeti kama ya kuandika katiba ya nchi iwe marufuku. Kuna kundi lina lengo la kuzuia katiba Mpya kupatikana. Kwa vyovyote vile lazima tuwashinde wapinga mabadiliko hawa kwa kuunganisha nguvu za wananchi. Tusirudi nyuma
"Forward ever, Backward never" - Nkrumah

suorce FB profile yake(ofisi ndogo)
My take;kiongozi muadilifu na mwanamapinduzi ya kweli huitaji torch kumtambua

kwa hiyo wenye msimamo wa serikali gani wanataka wanazuia mjadala? CHADEMA nao wana msimamo wa serikali tatu, nao wanazuia mjadala?
 
Kwani ZZK ameingia kwenye bunge la katiba kupitia kundi gani?
 
Si wa kwake, kwahiyo sisi tufanyaje? Nasi tunayo misimamo yetu.

Nadhani ZITTO alikuwa anawapiga kiaina Wahafidhina na msimamo wao wa serikali tatu, mwenywe anajua serikali tatu hazina maslahi kwa taifa.
 
Mimi msimamo wangu ni serikali moja, serikali tatu naona haina tija, ni mzigo tu.

Mimi nilikuwa mjumbe wa Tume ya Waryoba, huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Mwenyekiti wetu, lakini kutokana na pressure ya watu waliotumwa kwa malengo yao binafsi wakamzidi ujanja.
 
Zitto sioni anachokisema hapo. Ccm nitaasisi na ndio maana ina msimamo wake kama taasisi kwani mbona wasomi wa vyuo na wao wanamisimamo yao kuhusu serekali ngapi wana itaji. Hata zitto mwenyewe akilini mwake anamsimamo wake serekali ngap anaitaji.ata chadema waliwahikusema wanaitaji serekali tatu ndio wataotetea..
Ccm ni wa wazi ndio maana wametoa msimamo wao
 
bado kuna raia wanamfuatilia Zitto?
 
Zitto sioni anachokisema hapo. Ccm nitaasisi na ndio maana ina msimamo wake kama taasisi kwani mbona wasomi wa vyuo na wao wanamisimamo yao kuhusu serekali ngapi wana itaji. Hata zitto mwenyewe akilini mwake anamsimamo wake serekali ngap anaitaji.ata chadema waliwahikusema wanaitaji serekali tatu ndio wataotetea..
Ccm ni wa wazi ndio maana wametoa msimamo wao

Hata viongozi wa dini wanaitaka serikali mbili na huo ndiyo msimamo wao, CHADEMA hawawezi kuwa msimamo kwa sababu ni SACCOSS
 
Back
Top Bottom