Zitto - Msimamo wake kuhusu katiba mpya

Zitto - Msimamo wake kuhusu katiba mpya

Mimi nilikuwa mjumbe wa Tume ya Waryoba, huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Mwenyekiti wetu, lakini kutokana na pressure ya watu waliotumwa kwa malengo yao binafsi wakamzidi ujanja.
Kama hata wewe ulikuwa mjumbe huko, nasisitiza harufu mbaya ya kinye......
 
Hata viongozi wa dini wanaitaka serikali mbili na huo ndiyo msimamo wao, CHADEMA hawawezi kuwa msimamo kwa sababu ni SACCOSS
Pengo anataka kusimaia Ukatoliki Zanzibar, anajua kuliwa na serikali tatu Zanzibar itapiga marufuku Kutenai Ukatoliki , so anatetea mbili kwani zina maslahi kwa dini yake.........
 
Kwani ZZK ameingia kwenye bunge la katiba kupitia kundi gani?

kupitia wahafidhina wanaochakachua katiba yachama kusudi watawale milele huku wakimega vitu maalum na kutafuna ruzuku za chama.................
 
ccm ni makafiri

Unapanda basi la ubaguzi?! Watu au taasisi kama vyama vya siasa vinashindana kw hoja siyo matusi au dharau au chuki au ubaguzi wa aina yoyote Samaki Samaki. Mola atujalie tupate katiba yenye kuleta manufaa kw wote Tanzania. Mola bariki nchi ya Tanzania.Tanzania my motherland
 
Zitto sioni anachokisema hapo. Ccm nitaasisi na ndio maana ina msimamo wake kama taasisi kwani mbona wasomi wa vyuo na wao wanamisimamo yao kuhusu serekali ngapi wana itaji. Hata zitto mwenyewe akilini mwake anamsimamo wake serikali ngapi anahitaji.ata chadema waliwahi kusema wanahitaji serikali tatu ndio wataotetea..
Ccm ni wa wazi ndio maana wametoa msimamo wao
Mimi labda uelewa wangu uwa ni mdogo,nijuavyo CCM ndio chama tawala,kwa mujibu wa wao CCM ndio chama kinachowakilisha watanzania wengi,kwa mujibu wa maoni ya TUME YA WARIOBA Watanzania walio wengi wamependekeza mfumo wa serikali tatu.kama CCM ni chama kinachowakilisha Watanzania wengi basi impliedly CCM wanapendekeza muundo wa serikali tatu,sijui kama naeleweka
 
kwa hiyo wenye msimamo wa serikali gani wanataka wanazuia mjadala? CHADEMA nao wana msimamo wa serikali tatu, nao wanazuia mjadala?
Mbona unapenda kujitoa ufahamu wewe,Unaposema mfumo wa serikali 3 upo CHADEMA sidhani kama unatumia akili yako sawasawa kufikiri, Hii Rasimu iliyowasilishwa na TUME imependekeza Muundo wa Serikali Tatu na haya yote ni maoni ya wananchi ambao ni 64% ya waliotoa maoni yao mbele ya TUME hapo CHADEMA inaingiaje. kwa nini ukuitaja CUF, NCCR na vyama vingine wewe ni CHADEMA tu na usipoangalia utaolewa mwaka huu.
 
Zitto ana misimamo miwili tu: No posho na apewe uenyekiti CDM, basi. Hizi nyingine zote ni porojo.
 
Kauli ya zitto iko sahihi, ccm hawana dhamira ya dhati ya kupata katiba mpya, bali uchakachuaji wa mawazo ya wananchi!
 
Zitto ana misimamo miwili tu: No posho na apewe uenyekiti CDM, basi. Hizi nyingine zote ni porojo.

hapo kwenye uenyekiti panatia ukakasi,labda awe m/kt wa kikundi cha ngoma maarufu huku kwetu bugobogobo! kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi..
.......
 
Jamani eeh, misimamo ya kichama sisi haituitaki, hii katiba ni ya watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama, tusiendeshane kiitikadi hapa, msishindanishe vyama vyenu kwenye katiba yetu.Tunataka kila mtu awe huru kuchangia mawazo yake ili tupate katiba iliyo bora na sio bora katiba.Mnao kwenda kutetea vyama vyenu acheni kuchezea maisha ya watanzania mtatupeleka pabaya jamani.Nawaomba wajumbe wote wachangie mjadala huo kwa kuzingatia maslahi ya taifa na vizazi vijavyo. ASANTENI.
 
Zitto toka juzi anatafuta kuandikwa ila ANAPOTEZEWA.Dhambi ya usaliti ni mbaya.
 
kwa hiyo wenye msimamo wa serikali gani wanataka wanazuia mjadala? CHADEMA nao wana msimamo wa serikali tatu, nao wanazuia mjadala?

Acha upotoshaji kwenye maswala ya kitaifa, nadhani huu sio mjadala wa ccm v/s cdm ambao ndio una upeo nao. Msimamo wa serekali tatu ni wawananchi walio wengi kwa mujibu wa tume ya Jaji Warioba. Chadema ni kwamba na wao wanakubaliana tu matwaka hayo ya wananchi walio wengi. Acha utoto tafadhali.
 
Kila mtu ana msimamo wake, kura za maoni ndo zenyewe! bunge la katiba halima mashiko , watu wamekimbilia tu kula per diems, including wabunge wa Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi ZNZ ndo maana walilazimisha kuwa wajumbe!
 
Hata huku kuna uchama bado mngeteuliwa bado tungefanya ya kichama,tumuache yeye ya maoni yake.
 
Mbona unapenda kujitoa ufahamu wewe,Unaposema mfumo wa serikali 3 upo CHADEMA sidhani kama unatumia akili yako sawasawa kufikiri, Hii Rasimu iliyowasilishwa na TUME imependekeza Muundo wa Serikali Tatu na haya yote ni maoni ya wananchi ambao ni 64% ya waliotoa maoni yao mbele ya TUME hapo CHADEMA inaingiaje. kwa nini ukuitaja CUF, NCCR na vyama vingine wewe ni CHADEMA tu na usipoangalia utaolewa mwaka huu.

serikali tatu ni mzigo. muundo wa serikali ubaki hivyo hivyo serikali mbili, chadema wanataka serikali tatu ili wavunje muungano. shame on them...!!!
 
Back
Top Bottom