.
Ni kweli kabisa kuna ka bana mdogo kanaitwa nape kamepewa usemaji wa ccm na kujivika mamlaka ya m/kiti wa chama hicho. Ana mawazo yake binafsi ya serikali mbili na kwa hivyo ni haki yake na yanapaswa kuheshimiwa la katu katu watanzania tusikubali mawazo ya huyu ba mdogo kuwa ndio msimamo na absolute ya chama. Kajamaa haka ndiko kalikomshawiishi m/kiti na kumburuza katika wazo lake ili kuufanya kuwa ni msimamo wa chama.
Hivi tuwaulize ccm ni lini itafika waheshimu mauni ya wengi yaiopatikana kidemokrasia ya wengi wape? Wananchi tunauliza, kuna mungu mtu yupi ndani ya ccm anaetaka kujifanya kuwa yeye ndio katiba ya nchi? Jioneeni aibu enyi vizee vya ccm vyenye shingo ngumu na chonde chonde tunawaomba muyaheshimu mawazo ya wananchi wenu. Na kama hamtaki kuheshimu maoni ya wengi basi raia tutatumia njia mbadala kuwalazimisha kwa shurti kufanya hivyo.
.