kibokomchapaji
Senior Member
- Aug 18, 2017
- 165
- 307
Zitto kabwe amefilisika sana. Maneno yake kuhusu upungufu wa chakula nchini hayana mashiko.
Bodi ya Takwimu (NBS) ndio wa kwanza kusema kuna mfumuko wa bei.
Benki ya Dunia (WB) ikasema umasikini umepungua nchini hivyo watu wanamudu gharama za kununua vyakula.
Aidha, ripoti ya Utafiti wa kina wa WB inasema hakuna umasikini wa chakula kwani taifa lina chakula cha kutosha.
Katika uchumi wa sasa, serikali haifanyi ukiritimba hivyo serikali huwa na ghala lake, wafanyabiashara na wakulima huwa na maghala yao. WB ilitembelea kote humu na kukuta tani 341,136.41.
Zitto amechukua ripoti ya ghala moja na kujidanganya mwenyewe na wafuasi wake.
Mbaya zaidi, wakati WB inasema kilimo kimekua nchini na kutushauri tuimarishe kilimo, Zitto anasema tununue chakula.
Hatutaki serikali inunue chakula, Huu ndio utegemezi alioupinga baba wa taifa.
Mimi nadhani anatumiwa na mataifa yanayolima chakula kwa wingi kwa kutumia mbegu za GMO zenye madhara kwa afya.
Rashid Kilogi
Kigoma, Ujiji.