The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameahidi kuwa akichaguliwa hakuna mwanamke atakayelipa fedha wakati wa kujifungua.
Akizungumza leo katika Kata ya Buhanda, Kigoma, Zitto pia ameahidi kuboresha miundombinu ya barabara za kuunganisha Buhanda na mjini pamoja na mitaa ambayo kwa sasa ni mibovu na yenye makorongo. Amesema atajenga mtaro wa kupeleka maji Mto Mungonya ili kuokoa makazi ya wananchi.
Ameongeza kuwa miundombinu ya masoko ya jioni katika maeneo ya Kidagala na Mgeo itaboreshwa kwa kuweka pavements na taa, akisisitiza kuwa ana uzoefu wa kusimamia miradi hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata katika Soko la Marungu Mwanga.
Aidha, Zitto ameahidi kufuatilia kwa kina malalamiko ya wananchi kuhusu kunyimwa mafao na kuondolewa kwenye TASAF bila sababu za msingi.
Kuhusu gharama za ujenzi, amesema akichaguliwa bei ya saruji Kigoma haitazidi Sh 20,000 kwa mfuko wa kilo 50 kutokana na uwepo wa kiwanda cha saruji mkoani humo.