Zitto safarini Uingereza na Hispania

Zitto safarini Uingereza na Hispania

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614
Zitto ameondoka leo alfajiri kuelekea Uingereza na baadaye, Hispania. Taarifa ya Chadema iliyosainiwa na Ofisa Habari wake, David Kafulila imeeleza.

Kafulila amesema Uingeza ataongoza Kongamano la Mtandao wa Wabunge wanaoshughulikia migogoro ya kisiasa na usalama duniani, yeye akiwa Mwenyekiti Mwenza. Mwenyekiti wake nu Mbunge wa Ujerumani Angelika Beer. Kongamano hilo litaanza Machi 26 hadi Aprili 2, 2009.

Atarejea nchini Aprili 10 baada ya kwenda Hispania katika ziara ya wiki moja yenye lengo la kuhamasisha programu ya uendelezaji utalii mkoani Kigoma.

Kwa siku kadhaa Zitto amekuwa kimya kiasi cha kuanza kuelezwa kwamba leo angekuwa na Press Conference. Hakukuwa na Press Conf yoyote
 
Zitto ameondoka leo alfajiri kuelekea Uingereza na baadaye, Hispania. Taarifa ya Chadema iliyosainiwa na Ofisa Habari wake, David Kafulila imeeleza.

Kafulila amesema Uingeza ataongoza Kongamano la Mtandao wa Wabunge wanaoshughulikia migogoro ya kisiasa na usalama duniani, yeye akiwa Mwenyekiti Mwenza. Mwenyekiti wake nu Mbunge wa Ujerumani Angelika Beer. Kongamano hilo litaanza MAchi 26 hadi Aprili 2, 2009.

Atarejea nchini Aprili 10 baada ya kwenda Hispania katika ziara ya wiki moja yenye lengo la kuhamasisha programu ya uendelezaji utalii mkoani Kigoma.

Kwa siku kadhaa Zitto amekuwa kimya kiasi cha kuanza kuelezwa kwamba leo angekuwa na Press Conference. Hakukuwa na Press Conf yoyote

Huko Uingereza atakuwa anafadhiliwa na huo mtandao na huko Hispania je nani anamfadhili?

Je, Kafulila ndio nani? ni yule aliyeanguka katika gorofa? Je, Mbowe, Slaa, Tumbo, Mnyika, Komu na wengine wako wapi? Chadema semeni msikike
 
Kigoma Utalii poa! Ziwa, Wanyama N.k

Ila Miundombinu vipi?

Invest ktk miundombinu kwanza!
 
Awasalimie aendako, na pengine akirudi huo munuko wa KIDOWANS DOWANS utakuwa umepungua! mwe kijana huu mkenge sijui uliuvaaje masikini! Ila siku nyingine
ikikutokea kuwa muungwana ukiri kuteleza ( Kama alivo fanya mama Zakia wakati akiwa Waziri wa fedha baada ya kugundua Kagoda ni wizi akafuta barua yake)... kuliko kuzidi kulikoroga.
 
Mtu mwenye nia ya kupanda juu sometimes haangalii ni wapi ama nini anakanyaga,Mh Zitto maslahi yake kwa Tiafa ni mazito zaidi ya yale ya CHADEMA. Hilo la kufadhiliwa na matandao sina uhakika,hata hivyo huwa najiuliza sana maswali mengi pale mbunge wa upinzani anapopewa hishma kubwa na majukumu mazito na walioko madarakani,mara nyingi wao hubaniwa hadi wajitoe upinzani kama Kaborou,Marando,Lamwai nk.
Kitila Mkumbo naye majukumu yake yepi hayo?
Na Zitto naye Sangara hataki tena?
 
Afadhali ashughulikie pia mambo ya nyumbani (jimboni) kwake baada ya kujikita tu kwenye siasa za kitaifa zaidi
 
Ndiyo nilikuwa nasema hayo.. sasa sijui hiyo conference ilikuwa inafanyika kwa njia ya mnunurisho?
 
Ndiyo nilikuwa nasema hayo.. sasa sijui hiyo conference ilikuwa inafanyika kwa njia ya mnunurisho?

Nilizungumza naye jana, wala hakuwa na moango wa conference wala nini, na anasema hadhani kama anaweza kufanya press conference karibuni
 
Zito ana sumu ya mafisadi hawezi kuwageuka tena....heri aachane na siasa imemshinda....muda mfupi...du fisadis wana nguvu sana....
 
yap.

zito alisema maslahi ya taifa mbele. from there yeye aliona mitambo ya dowans ni bora ikinunuliwa. alikuwa anaogopa nchi kuingia gizan mwezi wa 4. mwez mvua za masika zinaponyesha

ni muhimu baadae tukija kuangalia mtizamo wake ule kama ulikuwa the best solution for the power problem. manaake sie siku zote tuna limited resources (pesa etc.) kwa hiyo siku zote tunatakiwa tutoe pesa kugharamia the best solution available. sio mradi tumenunua

mungu aijalie safar yako. tuna vivutio vingi havijulikan
 
Atarejea nchini Aprili 10 baada ya kwenda Hispania katika ziara ya wiki moja yenye lengo la kuhamasisha programu ya uendelezaji utalii mkoani Kigoma.

Hispania ni nchi mojawapo maskini wa mwisho katika nchi za Western Europe.Malofa wale watasaidia nini cha maana mkoa maskini wa Kigoma? Wahispania wengi ni malofa hata kutalii kwao ni luxury ambayo hawawezi ku-afford.Tanzania ukimwona mtalii toka hispania ni ndoto.

Zitto kaanza usanii kama ni kuhamasisha ni heri angeenda Uingereza au ujerumani au marekani.Hispania anatufunga kamba ni usanii usiosaidia Kigoma labda awe anaenda kule mwenyewe kutalii kwenda kuangalia ulofa wa wahispania aende akawasimulie maskini wa Kigoma.Hatarudi na cha maana cha hiyo programme toka Hispania.
 
Msimamo wa mwanakijiji kwa Zito unanitia shaka kwani, swala la kuteleza na si kuanguka sielewi.
Zito haitetei Dowans kimakosa anajua nini anakifanya na wala hakuteleza.
Huwezi kutaka mabadiliko na kutaka kutetea uvunjwaji wa sheria. Ni kweli Zito kanunuliwa, na kama kina Lamwai, Marando, Kaboru nk Zito yupo mbioni kuelekea dampo.

Chadema wanatakiwa kuwa smart na kuligundua mapema kabla ya madhara zaidi. Kwanza ametupunguzia kasi yetu big time. Pili kamchachisha sangara.
 
yap.zito alisema maslahi ya taifa mbele. from there yeye aliona mitambo ya dowans ni bora ikinunuliwa. alikuwa anaogopa nchi kuingia gizan mwezi wa 4. mwez mvua za masika zinaponyesha

Nchi imeshaanza kuingia giza wiki moja hata kabla ya 1 Aprili, siku ya wajinga duniani!
 
... Ila Miundombinu vipi?
Invest ktk miundombinu kwanza!

Miundombiinu ni pamoja na umeme. Kule Kigoma hawajaunganishwa katika gridi ya taifa. Kama ingenunuliwa mitambo mipya walau ingekuwepo hoja ya kuunganisha Kigoma katika gridi. Kwa sasa mtu hawezi kuzungumzia kuongeza "load" au mzigo katika vyanzo vya umeme vilivyopo, wakati hata mzigo uliopo unaelekea pabaya. Ipo siku majenereta ya umeme "yatatema mzigo" na hapo ndipo watu watakapoanza kuitafuta mitambo mipya, au walau ya Dowans. Tuliosoma Electrical Power tunaelewa hivyo, na tulifundishwa hivyo. Nadhani wengi hawakumuelewa Zitto pamoja na Serunkamba.
 
I salute you Mh Zitto,

Wewe ni kiongozi bora kijana ambaye wengine wanatakiwa waige mfano wako. Nimefuatalia mada ya hivi karibuni, nimekubali kuwa una msimamo na unaelewa nini unachokisema. Ni dhahiri kabisa katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yako kama mwakilishi wa wananchi (mbunge) umekuwa ukizingatiia maslahi zaidii ya Taifa lako na si vinginevyo. Japokuwa mimi ni CCM, lakini ningependa kuona tunaendelea kuwa na viongozi wazuri wa wananchi bila ya kujali wanatokea chama gani. Kuwepo kwenu kunaipa changamoto CCM katika utekelezaji wa majukumu yake.

Ninakutakia safari njema na mungu akurejeshe salama.
 
Tunaye Mh. Zitto mmoja ambaye hatujui labda huko mbele ya safari anaweza kutugeuka, ila ninatoa shime wanajamii tuandae vijana wengi zaidi ktk maadili ya taifa wenye kujali na utaifa. Unajua nachelea how dissapontment itakavyokuwa endapo tutatumia kmjenga ZITTO mmoja halafu akakengeuka....
 
Back
Top Bottom