Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015


karibu kwenye kufundisha Kamanda Zitto...karibu sana
 
For sure hawa wanafunzi wa chuo wamerogwa.. eti january namba moja then mnyika namba tatu.. hivi wameona hii nchi ni yakuchezea ndio maana graduates wengi wanapata tabu kupata kazi sababu akili zao ndogo..
 
Dr.W.Slaa atapumua sara manake usingizi walikuwa hawaupati na Ben Saanane atapumzika katika kazi aliyokuwa amepewa na slaa. SUMU itapa pumziko sasa.

Mbona haya madai yako huyapeleki kwenye nvyombo vya usalama hili wachukuliwe hatua? alaf wewe ndiye unaye lalamika kuliko unayemsemea? mbona mwenyewe aliwakana? amchoki?
 
Kutokana na principles of demand and supply, habari hii itasababisha bei ya sumu madukani kushuka.
Yaani ninavyotamani kukuona wewe na washirika wako wa lumumba nijue mnaonekanaje yaani nashindwa kuelewa kama nanyi ni binadamu wa kawaida kweli.
 
i wonder!! Inakuwaje ma ccm waumie na kulalamika as if wao ndiyo wameumia kuondoka kwa zito so its true ana faida kwenu kuliko kwa wana cdm? Kama ni hivyo bora aende tu.

zitto aliondokaga cdm kitamboooo!usishangae akaibukia rasmi umagambani!Au mshauri wao nyuma ya pazia.niliwahi kusikiaga alikuwa anawasiliana na tiss na arosto.kwa siku za karibuni alikaa kimagamba zaidi!!!!sijui nini kilimkwaza huko cdm.mwenye kujua atujuze.he is a controversial figure after all.
 

Unaongea kama umefumaniwa na kichaa
 
Zitto ahaminiki anapenda kutajwatajwa na kuandikwa,alisema atakua mbunge wa maramoja 2005,ilipokaribia uchaguzi 2010 akadai majimbo kumi yamemuomba agombee,baadae akadai Kigoma kask ameombwa na wazee aludi tena,Tusubiri 2015 september Tuone,yupo wapi Ramadhan Semtawa
#Ex Tanzania Simper aliquid novi#
 

mkuu THE BIG SHOW kwa nini ushindwe kujadili mada ujadili watu? hivi umesoma comment zako toka mwanzo wa huu uzi? kwa nini tusijadili mada tujadili watu? kwa nini huu tusiufafananishe na uchonganishi? unadhani unajadili mada lakini unajadili watu wasio husika.
Kwa nini tuwatukane watu kisa wanawapenda tusio wapenda? kwakweli kama mtu atafatilia comment zako kwenye uzi huu na unapotoa like atajua tuu wewe ni mtu wa namna gani.

huu uzi umeletwa kutuhabarisha si kudharauriana, ni bora tuundelee kuwaheshimu hata ambao atuwapendi. hivi kweli tunajiita wanachadema huku tukiside na maadui na kushare silaha zilezile wanazotumia kutumaliza? aiseeee
 
Last edited by a moderator:
Hii habari inaweza kuwa ni yakutungwa
 

Sasa Ben Saanane na Yericko ndiyo waliomtuma zitto kufanya mawasiliano haya na Rostam Aziz na Jack Zoka waliochakachua uchaguzi mkuu uliopita huku Zitto mwenyewe akihusishwa kuhujumu baadhi ya wanasiasa vijana?Kwa maelezo haya haya hapa chini Zitto alikua akifanya yake?

[h=2][/h]
''ZITTO Kabwe, naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amekuwa na mawasiliano ya karibu na na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, imefahamika.
Kufichuka kwa taarifa za mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha mawasiliano kati ya Zitto na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka.
Aidha, kufichuka kwa mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja siku mbili baada ya mama mzazi wa Zitto, Shida Salum kunukuliwa akisema, “Mwanangu ni mkorofi.”
Mama Zitto alikieleza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, “Namfahamu mwanangu. Ni mkorofi. Si msikivu.”
Kwa mujibu wa rekodi ya mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini, TISS na Rostam, watu hao wawili wamekuwa wakijadiliana mambo kadhaa.
Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na viongozi hao, yanahusu CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taifa kwa ujumla.
Rostam ambaye CHADEMA imekuwa ikimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi, ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM.
Gazeti hili limeshindwa kujua mapenzi ya Rostam kwa CHADEMA hadi kujipa jukumu la kujadiliana na Zitto juu ya “uhai bora” wa chama hicho.
Kwa mfano, Zitto na Rostam walifanya mawasiliano ya simu mara tano hapo tarehe 11 Agosti 2010. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754555555 ambayo hutumiwa na Rostam.
Mawasiliano hayo yalifanyika saa 07:08:35, saa 22:09:02, saa 22: 28: 39, saa 22:49:54, saa 22:44:37 na saa 22:45:09.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika simu ya Zitto ilikuwa inasomeka kuwa yuko Uzunguni, Dodoma, huku simu ya Rostam ikisomeka kuwa ilikuwa Area D, Dodoma.
Mawasiliano mengine yalikuwa katika maeneo tofauti. Mathalani mawasiliano ya Zitto na Rostam yalyofanyika 30 Novemba 2010 yalionyesha kuwa Zitto yuko Ohio, Ilala, Dar es Salaam. Yalifanyika saa 14:58:42, saa :16:41:58, saa 15:38:00, saa 16:09:56 na 17:48: 35.
Mawasiliano mengine ya Zitto na Rostam yalifanyika siku mbili kabla ya wabunge wa CHADEMA hawajakutana Bagamoyo.
Mawasiliano hayo yalifanyika tarehe 7 Desemba 2010 saa 07: 57:27, saa 14:32:08, saa 09:44:36 na saa 14:07:07.
Haijaweza kufahamika pia kiini cha mawasiliano kati ya Zitto, Zoka, Rostam na vigogo wengine wa serikali, CCM na usalama wa taifa.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya kikao cha CHADEMA, awali mama Zitto alieleza masikitiko yake kuhusiana na taarifa mbalimbali zinazomhusu mwanawe.
“Najua mwanangu ni mkorofi. Lakini kuna njia ya kufanya kuliko kukitia chama msukosuko…Kila mara Zitto, Zitto, Zitto. Haya mambo hayana faida kwa chama,” alieleza.
Hata hivyo, vyanzo huru vya taarifa vimeeleza MwanaHALISI kuwa mpango uliopo ni kumtumia Zitto “kusambaratisha CHADEMA.”
“Kaka, nakuhakikishia kuwa upo ushahidi wa kutosha kwamba Zitto anatumika kuvuruga CHADEMA. Kuna baadhi ya vigogo ndani ya CCM na serikali, wanaomtia ujinga kwa kumueleza, ‘kwa hali ilivyo ndani ya CCM, wapo baadhi ya watu wanatamani kuondoka. Lakini hawawezi kwenda CHADEMA kwa sababu kinaongozwa na Mbowe (Freeman Mbowe),’” ameeleza mtoa taarifa.
Anasema, “Hivyo wanampampu Zitto kugombea uenyekiti. Wanataka Mbowe ang’oke na CHADEMA kisambaratike. Ni kwa sababu, wote wanaomtumia Zitto, wanajua kuwa huyu bwana mdogo hana uwezo wa kuongoza CHADEMA na haaminiki.”
Akiongea kwa kujiamini, mtoa taarifa anasema, “Ni mbinu zilezile zilizotumiwa NCCR- Mageuzi, ambapo baadhi ya vigogo wa idara ya usalama wa taifa walitumia fedha ili kumng’oa Marando (Mabere Marando), katika uongozi wa chama.”
Anasema taarifa kwamba wapo watu wanataka kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ni mkakati unaosukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya vigogo wa serikali kwa kushirikiana na usalama wa taifa.
Inadaiwa ni katika mkakati huo, ndimo linapatikana jina la Rostam ambaye uongozi wa juu wa chama hicho umekuwa ukimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.
“Unajua ndugu yangu hapa Tanganyika, Rostam angependa sana awe na uwezo wa ku-control vyama vyote vinavyokua, hasa CHADEMA kwa sasa; ingawa uwezo wake wa kupenyeza unakuwa mgumu.
“Mkakati wake ni kumweka mtu wao katika uongozi wa juu wa CHADEMA ili waweze kumuendesha. Mpango huo ukifanikiwa, kina RA (Rostam) wataacha ugomvi na CHADEMA. Kwa sasa mtu wao ni Zitto. Na kuna mambo mengi ya siri ambayo RA amekubaliana na Zitto,” anaeleza mtoa taarifa mmoja ambaye yuko karibu na Rostam na Zitto.
Mjadala juu ya mwenendo wa mashaka wa maisha ya kisiasa ya Zitto, uliibuka baada ya katibu wa wabunge wa CHADEMA, John Mnyika kuwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo mbele ya Kamati Kuu.
Kikubwa kilichojadiliwa ni hatua ya Zitto kuongoza kikundi cha baadhi ya wabunge kusaliti maamuzi halali ya kamati ya wabunge wa chama hicho.
Zitto anatuhumiwa na wabunge wenzake kutotii agizo la kutoka nje wakati Rais Jakaya Kikwete anahutubia Bunge, 18 Novemba 2010.
Katika taarifa yake kwa CC, Mnyika alisema katika kushughulikia suala hilo, hakukuwa na lolote la kuviziana kama ambavyo baadhi ya wajumbe wamedai.
“Hakuna kanuni iliyovunjwa, wala hakuna kinachoitwa kuviziana. Wabunge walikuwa na hasira sana juu ya hatua ya Zitto na wenzake kutotii agizo la kamati na kupita katika vyombo vya habari kupotosha ukweli,” alisema Mnyika kwa sauti ya upole.
Akiongea kwa sauti ya kusisitiza, Mnyika alisema, “Mheshimiwa mwenyekiti, kwa kweli, wabunge walitaka hata kuwapiga wabunge walioasi makubaliano yao. Uongozi wa Kambi ukafanya juhudi kulipeleka mbele suala hili, angalau kupunguza munkari wa wabunge,” alieleza.
Ni katika kikao hicho cha wabunge kilichofanyika Bagamoyo, ndipo wabunge walipiga kura ya kutokuwa na imani na Zitto.
Kile kilichoitwa, “kuviziana” kiliibuliwa ndani ya kikao cha CC na Dk. Kitila Mkumbo, ambaye amenukuliwa akisema ameshutushwa na hatua ya wabunge kumhukumu Zitto wakati ni mgonjwa.
Alikuwa ni Benson Kigaila, mjumbe wa CC aliyeeleza viongozi wenzake umuhimu wa kujenga chama imara badala ya kuangalia mtu.
“Mtu aliyekosea, lazima aadhibiwe. Tusiangaliea kama ataanguka, au atanufaika. Kwa muda mrefu, chama hiki kimenufaika kwa makosa ya CCM, ambapo kutokana na makundi yanayokinzana, wameendelea kukumbatia maovu. Ni lazima chama kichukue hatua za kukabiliana na magenge haya,” alieleza.
Mjumbe mwingine wa CC aliyeongea kwa sharti la kutotajwa gazetini, ameliambia gazeti hili, “Yale mambo yalikuja kama taarifa, si vingenevyo. Jukumu sasa, liko kwa Zitto mwenyewe kujipima kama anaweza kuongoza watu ambao hawana imani naye.”
Baada ya kupeleka taarifa hiyo CC, wabunge wameeleza, “…Tunapeleka maamuzi yetu haya kwa Zitto. Anatakiwa kuamua ama kuachia ngazi au kusubiri hatua nyingine zinazofaa kuchukuliwa kwa mtu kama yeye katika kikao chetu kingine.”
Mara baada ya mjadala wa Zitto kwa CC kutoingilia maamuzi ya Kamati ya wabunge wake, ndipo uamuzi wa kuunda kamati ndogo ya “kumpa ushauri” Zitto ilipoundwa.
Kamati hiyo inaongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.Wajumbe wake ni Nyangali Shilungushela, SylivesterMasinde na Mama Zitto.
Kazi ya kamati ya Baregu ni kufuatilia nyendo za Zitto, kumshauri jinsi ya kujibadilisha ili hatimaye arejee katika nji''
 


gombea kwanza urais mkuu,ikishindikana ndio uondoke,kura yangu ipo kwa ajili yako mh zzk
 
hata ungegombea usingepata huo urais...mwinyi,JK halafu wewe? nani atakubali mambo haya
 
kiongozi mbona unaleta zilipendwa au nawe wale wale wa kutembea na sumu mfukoni?
 
Kuitumikia Tanzania sio razima uwe mwanasiasa,unaweza kuitumikia Tanzania kwa namna nyingine na mchango
wako ukaonekana kwa Taifa.
 

Stop being paranoid ......
I dont give shit about Chadema,i care about opposition to be strong which is not that strong .
CCM kupitia njia nyingi inatokomeza upinzani nchini ,CCM ndio serikali kwa kipindi vyama vingi vinaanzishwa ilitakiwa kuhakikisha upinzani unakomaa na unakuwa wa kupishana sera zaidi ya tunayosikia sasa wizi/ufisadi kitu ambacho chama chochote kinaweza kuwa .Kwa kuwa viongozi ni product ya wananchi bila mentality ya wananchi kubadilika basi hata viongozi awaye toka chama chochote anaweza kuwa wizi.

Katika haya yote still Chadema kimejitahidi kiasi fulani kuonyesha upinzani (kidogo nimesikia sera zao ingawa still ajenda kuu imekuwa si sera ni janga la ufisadi linalo sumbua nchi) ,katika hili akatokea mtu ambaye anadaiwa kushiriki kuchenga chama na mtu huyo in downlow kutumika kudhoofisha chama ,is a big TRAITOR. no matter how good is he ,but i art of war this guy hafai kwa chumvi wala kwa sukari.

Kama wewe ni shabiki tuu hutajua usaliti wake maana sizungumzii ktk level ya sijuhi kutoshiriki mikutano au maandamano ,nazungumzia mikakati na vikao kitu ambacho mwenyewe na baadhi ya CCM wanajua.They got him!!Hkuna siri inayohusisha group....
 


Hao unaohis wewe kuwa tunawajadili au tuna wa-attack ndio wanaojenga taswira mbovu kwa chama,na ndio wanaosababisha choko choko,huku wakidhani kama wao wana influence kwenye chama na kwenye jamii,ili hali hao si kitu,hakuna anaewafaham,hakuna walilolifanya la kuzingatiwa,nadhan wamefikia hatua ya kuota pembe na kuhis labda wana influence,wana followers na wana sikilizwa,thats why sisi tunawaambia wafute hizo notions vichwani mwao,na waanze kuish maisha yao,wasitegemee kwamba kuna shortcut maishani,
Hiyo ndiyo point yangu,hakuna chuki,hakuna kujadili mtu,na kiukweli siwapendi kutokana na kuendekeza kwao njaa,
Thanks kama umekuwa unanifuatilia kwa karibu,naomba sasa uelewe mantiki ya hoja zangu kwa hao watu njaa kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…