Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Mkuu mbona umechoka haraka kabla hujawakomboa watanzania?au umemaliza kazi uliyotumwa naCCM ya kukidhoofisha chadema?Mkuu we we ni msaliti Wa upinzani
 
zito yuko vzr sn ila amepata suprising atack namuunga mkono astaafu tu aangalie upande wa pili wa shilingi
 
wanasema kila kitu huanza na ndoto ila huyu mtoto wa makamba naona anaota mchana kweupe. sijui usiku ataota ndoto hiyohiyo ya urais?
 
wanasema kila kitu huanza na ndoto ila huyu mtoto naona anaota mchana kweupe. sijui usiku ataota ndoto hiyohiyo ya urais?

Ubunge wenyewe umemshinda, urais ndio atauweza....zito ni janga la taifa. ..kikwete ameshusha hadhi ya urais
 
Kama ndivyo basi amewajib CDM na amewaelewesha watanzania wasio yaelewa kuhusu Zitto,Pumzika kijana ila angali tunakuhitaji ktk siasa tena.
 
Hivi ni nani aliyekudanganya kuwa Zito anaweza kuwa lecturer. Wewe unafikiri kuwa lecturer unaamka tu na kusema nataka kuwa lecturer? Labda kama ni kile chuo cha Morogoro ambacho kina wakuu wa idara wenye masters degree za arabic halafu anakuwa mkuu wa kitengo cha lugha.

Zito anatangatanga na degree za kuungaunga halafu akawe lecturer? Degree yake inayotambulika hasa ni moja tu aliyoipata UDSM. Nyingine zimekaa kisiasa zaidi.

ZZK anafaa kupewa wizara moja nyeti aiendeshe from 2015..!! Huhitaji kuwa lecturer kwa sasa wkt bado kijana hivi..!! utafundisha tu uzeeni bado utakua haujachelewa but kwa sasa taifa linakuhitaji sana..!!
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.


Source: Majira


Kila nafasi anaona haina hadhi yake
 
Upo sahihi kabisa. Ukiona mtu anafahamika sana na kila mmoja anataka kuchangia ni lazima huyu mtu awe maarufu sana. Umaarufu huo unaweza kuwa wa uovu kama ulivyokuwa wa Hitler, Ascoba, Noriega, Rage, n.k. au unaweza kuwa ni umaarufu wa mambo mema, umaarufu wa kupendwa kama ule wa Mandela, Mwalimu Nyerere, Princes Diana, n.k. Sasa Zito ni umaarufu wa kupendwa au kuchukiwa?

"zitto is a great man" haiwezekani mtu mdogo atawale habari za mitandao ya kijamii kila kukicha kama mtu huyo siyo tishio.
 
Tatizo la zitto ni uzalendo wake anaipenda sana nchi yake na tatizo lake ndyo hilo ....laiti km angejifunza unafki Wa kukaa kimya hta km kuna maovu yanatendeka mpk Leo angekuwa shujaa
 
Ubunge wenyewe umemshinda, urais ndio atauweza....zito ni janga la taifa. ..kikwete ameshusha hadhi ya urais

tatizo brainwash ndyo zinawasumbua na kufata mkumbo zitto ni chhadema damu kuliko wakina lisu na sugu sema kukataa kwake unafki ndyo kumemponza
 
Zitto kinachomponza na sehemu atokayo,dini yake na kabila lake ingekuwa ni mchaga,mkristo au kutoka kaskazini tayari angeshakuwa mwenyekiti wa Chadema, na mpigiwa debe kuliko mtu yeyote yule Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Zitto kinachomponza na sehemu atokayo,dini yake na kabila lake ingekuwa ni mchaga,mkristo au kutoka kaskazini tayari angeshakuwa mwenyekiti wa Chadema, na mpigiwa debe kuliko mtu yeyote yule Tanzania.

Na wewe kinachokuponza ni nini ?
 
Last edited by a moderator:
zitto ni kiongozi na ili anahitajika but iwe ndani ya chadema,..nje ya chadema atakuwa amesaliti chadema ambayo yeye ameitumikia sana.
 
Back
Top Bottom