Kumbe kila kitu hasemi ukweli.Hatendi ukweli. Kazi ni kujichora tu kuwa yu sahihi muda wote;mpambanaji;mfuata Kanuni;anayefuatwafuatwa;anayesemwa vibaya;anayenyanyaswa na kadhalika. Kumbe, wapi! Leo Tanzania imeambiwa 'ukweli'. Ukweli kuwa Zitto anafanya maigizo tu kuhusu mabilioni ya Uswisi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jaji Fredrick Mwita Werema na William Lukuvi,kama nilivyowataja, 'wamemuanika' Zitto.
Wakichangia kwa kufuatana, Werema na Lukuvi wamesema kuwa Zitto hana hata jina moja la walioficha mabilioni Uswisi-hoja anayoishupalia Zitto kila uchao. Wakasema kuwa Zitto, kwa kiapo (Affidavit) ametamka na kuthibitisha kuwa hana hata jina moja la mficha-mabilioni Uswisi. Mimi siamini!
Kumbe Zitto ni mtu wa utani hivi kwa watanzania!?? Hoja amewasilisha Bungeni;amekutana na viongozi mbalimbali wa kidunia kuhusu suala hili;amesafiri kwenda Ujerumani mara kadhaa kwa suala hili na kadhalika. Kweli atubabaishe wakati wote huo? Siamini.
Kama Zitto amechokozwa leo (na tena amedhalilishwa), umefika muda wake kujibu mapigo. Kutaja majina ya waficha-mabilioni Uswisi. Hana haja ya kumpa Godbless Lema. Ataje mwenyewe. Muda ni huu.Akishindwa, tutamuona muongo sana. Atakuwa hafai (na kutamka kimatendo kuwa hautaki) Urais wa nchi hii wala Uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA.
CCM 'tumembeep', kama anaweza atupigie!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam