Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe kila kitu hasemi ukweli.Hatendi ukweli. Kazi ni kujichora tu kuwa yu sahihi muda wote;mpambanaji;mfuata Kanuni;anayefuatwafuatwa;anayesemwa vibaya;anayenyanyaswa na kadhalika. Kumbe, wapi! Leo Tanzania imeambiwa 'ukweli'. Ukweli kuwa Zitto anafanya maigizo tu kuhusu mabilioni ya Uswisi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jaji Fredrick Mwita Werema na William Lukuvi,kama nilivyowataja, 'wamemuanika' Zitto.
Wakichangia kwa kufuatana, Werema na Lukuvi wamesema kuwa Zitto hana hata jina moja la walioficha mabilioni Uswisi-hoja anayoishupalia Zitto kila uchao. Wakasema kuwa Zitto, kwa kiapo (Affidavit) ametamka na kuthibitisha kuwa hana hata jina moja la mficha-mabilioni Uswisi. Mimi siamini!
Kumbe Zitto ni mtu wa utani hivi kwa watanzania!?? Hoja amewasilisha Bungeni;amekutana na viongozi mbalimbali wa kidunia kuhusu suala hili;amesafiri kwenda Ujerumani mara kadhaa kwa suala hili na kadhalika. Kweli atubabaishe wakati wote huo? Siamini.
Kama Zitto amechokozwa leo (na tena amedhalilishwa), umefika muda wake kujibu mapigo. Kutaja majina ya waficha-mabilioni Uswisi. Hana haja ya kumpa Godbless Lema. Ataje mwenyewe. Muda ni huu.Akishindwa, tutamuona muongo sana. Atakuwa hafai (na kutamka kimatendo kuwa hautaki) Urais wa nchi hii wala Uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA.
CCM 'tumembeep', kama anaweza atupigie!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Jamani urafiki wako na Zitto umekatika ghafla hivi! Kweli kabla mwaka huu haujaisha tutasikia na kuona maajabu mengi!Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.
Nyie watu wekeni akiba mtakosa pakujificha. Yaani hawa akina AG na LK mmewaamini ghafla? Kwa hiyo kesho wakiwaambia ule mkanda wa mabomu ya Arusha ni feki, haupo mtakubali na kuwashangilia?
zitto alishtukiwa siku nyingi na watanzania.hata kwenye daladala wanamsema vibaya sana huyu mtu.nawashangaa wahariri wanavyomwandika kwenye kurasa za mbele za magazeti yao kila uchao.hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uandishi wa habari ulivyo chini hapa tanzania.uandishi kabila hii ni janga kwa hakika.
Mwenzako ameitwa Ikulu ndogo kuulamba uwaziri, wewe endelea kusema anafanya utani utani
Nyinyi mnafikiri nguvu ya mafisadi mchezo!-Usipoenda polepole na kwa umakini Mkubwa wanakutoa roho!.
Nampa Big up sana Zitto Kabwe, Furaha ya Askari Makini ni Kushinda vita na Ukabaki hai!. TUMUUNGE MKONO ZITTO, ANGALAU ANATHUBUTU, KUTAJIWA MAJINA HALAFU MFUMO UKABAKI PALEPALE NI UJINGA!. JE LISTI YA MWEMBE YANGA HATIMAYE ILIMSAIDIA NINI MNYONGE?. NI LAZIMA TUPIGANIE KUBADILI MFUMO.
KUTAJA MAJINA NI KITU CHEPESI KULKO KUBADILI MFUMO, NA MAADAM USWISS WAMEKIRI KUWA KUNA WATU WANA VIJISENTI HUKO VINGI TU, NI BORA SERIKALI IKACHUKUA HATUA, BADALA YA KUMUATTACK WHISTLE BLOWER YAANI ZZK.
hata hakitaja bado mtampinga tu maana jayari mnamwita msaliti
Ataje anayo?
Kumbe kila kitu hasemi ukweli.Hatendi ukweli. Kazi ni kujichora tu kuwa yu sahihi muda wote;mpambanaji;mfuata Kanuni;anayefuatwafuatwa;anayesemwa vibaya;anayenyanyaswa na kadhalika. Kumbe, wapi! Leo Tanzania imeambiwa 'ukweli'. Ukweli kuwa Zitto anafanya maigizo tu kuhusu mabilioni ya Uswisi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jaji Fredrick Mwita Werema na William Lukuvi,kama nilivyowataja, 'wamemuanika' Zitto.
Wakichangia kwa kufuatana, Werema na Lukuvi wamesema kuwa Zitto hana hata jina moja la walioficha mabilioni Uswisi-hoja anayoishupalia Zitto kila uchao. Wakasema kuwa Zitto, kwa kiapo (Affidavit) ametamka na kuthibitisha kuwa hana hata jina moja la mficha-mabilioni Uswisi. Mimi siamini!
Kumbe Zitto ni mtu wa utani hivi kwa watanzania!?? Hoja amewasilisha Bungeni;amekutana na viongozi mbalimbali wa kidunia kuhusu suala hili;amesafiri kwenda Ujerumani mara kadhaa kwa suala hili na kadhalika. Kweli atubabaishe wakati wote huo? Siamini.
Kama Zitto amechokozwa leo (na tena amedhalilishwa), umefika muda wake kujibu mapigo. Kutaja majina ya waficha-mabilioni Uswisi. Hana haja ya kumpa Godbless Lema. Ataje mwenyewe. Muda ni huu.Akishindwa, tutamuona muongo sana. Atakuwa hafai (na kutamka kimatendo kuwa hautaki) Urais wa nchi hii wala Uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA.
CCM 'tumembeep', kama anaweza atupigie!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.
Wewe ndio ulikuwa unampamba ukizani ana lolote ni kwamba hana lolote na hata akienda chama chochote ataishia kuwa mtu wa migogoro tu.Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.