Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Ndg. Zitto kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo akiongea na wananchi wa Kagerankanda, Kasulu vijijini amedai kuwa walimwekea mtego wa rushwa afisa wa Wakala wa Misitu Tanzania
Katika msitu wa Makere Kusini ukiitizama mipaka iliyokuwepo mwaka 1956 na hivi sasa pori la akiba limeingia kwenye maeneo ya Wananchi. Wananchi wamekosa maeneo ya kufanya shughuli zao za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na urinaji wa asali. Kutokana na hali hii wananchi wamekuwa wakipigwa na kuumizwa na askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) ikiwemo kuporwa mazao yao.
Nimemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii kuchukua hatua mara moja dhidi ya Mkuu wa TFS (Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania) Kasulu na maafisa wengine wote. Vyombo vya uchunguzi wa jinai vichukue hatua dhidi ya wezi hawa, wafikishwe mahakamani.